Korea Kaskazini: Tunaweza kushambulia eneo lolote Marekani

Kombora hilo lililorushwa nyakati za giza alfajiri siku ya Jumatano lina uwezo mkubwa kushinda kombora lolote lile a taifa hilo



Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionKombora hilo lililorushwa nyakati za giza alfajiri siku ya Jumatano lina uwezo mkubwa kushinda kombora lolote lile a taifa hilo

Korea Kaskazini imesema kuwa imefanikiwa kulifanyia majaribio kombora lake la masafa marefu ambalo linaweza kufika eneo lolote la Marekani.
Runinga ya kitaifa nchini humo imesema kuwa Pyongyang sasa imefanikiwa kuafikia azimio lake la kuwa taifa lenye nguvu za kinyuklia.
Kombora hilo kwa jina Hwasong-15 ambalo imesema ndio kombora lenye uwezo mkubwa lilirushwa katika giza mapema siku ya Jumatano.
Lilianguka katika maji ya Japan lakini liliweza kuruka juu zaidi ya kombora jingine lolote la taifa hilo .
Kitengo cha habari cha taifa hilo KCNA kilisema kuwa kombora hilo liliruka katika kimo cha kilomita 4,475 na kusafiri kwa umbali wa kilomita 950 katika dakika 53.
Kombora hilo lililofyatuliwa kwa mwinuko halikupitia katika anga ya Japan kama makombora mengine hapo awali na lilianguka kilomita 250 karibu na pwani yake ya kaskazini , kulingana na maafisa wa Japan.


Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong un alishuhudia kurushwa kwa kombora hilo
Image captionKiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong un alishuhudia kurushwa kwa kombora hilo

KCNA imeongezea kuwa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un ambaye alishuhudia kufyatuliwa kwa kombora hilo alitangaza 'kwa majivuno' kwamba sasa tumekamilisha lengo letu la miaka mingi la kuwa taifa lenye nguvu za kinyuklia.
Ripoti hiyo imesema kuwa kama taifa lenye nguvu za kinyuklia na linalopenda amani, Korea Kaskazini itafanya kila iwezalo kutekeleza lengo lake la kuleta amani na udhabiti duniani.
Imesema kuwa, silaha zake za ulinzi dhidi ya sera ya kibepari ya Marekani, hazitatishia taifa lolote duniani iwapo maslahi ya Korea Kaskazini hayatakiukwa.''Hilo ndio tangazo letu''

Comments

Popular posts from this blog

Jifunze Jinsi ya kutengeneza sabuni ya Unga na ya maji

Mkataba wa Aishi Manura wavuja ukionyesha kujiunga na simba Simba

Antoine Griezmann: Nyota wa Atletico Madrid aomba radhi baada ya kujifanya mweusi