Korea Kaskazini yarusha kombora 'lililoruka juu zaidi'

Waziri wa ulinzi nchini Marekani James Mattis amesema kuwa kombora hilo linaweza kufika mahala popote pale duniani


Image captionWaziri wa ulinzi nchini Marekani James Mattis amesema kuwa kombora hilo linaweza kufika mahala popote pale duniani

Taifa la Korea Kaskazini limefanyia majaribio kombora lake la masafa marefu lililoruka juu zaidi na kombora hilo tayari limeonekana kuhatarisha usalama duniani kulingana na waziri wa maswala ya ulinzi nchini Marekani James Mattis.
Jaribio hilo la kombora mapema siku ya Jumatano lilianguka katika maji ya Japan.
Liliruka kwa urefu wa kilomita 4,500 na kusafiri umbali wa kilomita 960 kulingana na jeshi la Korea Kusini.
Ni jaribio la hivi karibuni ambalo limezua hali ya wasiwasi.
Mara ya mwisho kwa taifa hilo kulifanyia jaribio kombora lake ni mwezi Septemba.
Wakati huo, kombora lake la mwisho lilikuwa la sita la nguvu za kinyuklia mwezi huo.

Gwaride la kijeshi la taifa la Korea Kaskazini
Image captionGwaride la kijeshi la taifa la Korea Kaskazini

Korea Kaskazini imeendeleza mpango wake wa kinyuklia pamoja na ule wa utengenezaji wa makombora licha ya shutuma kutoka kwa jamii ya kimataifa.
Baraza kuu la usalama la umoja wa mataifa linatarajiwa kukutana katika kikao cha dharura ili kuzungumzia hatua hiyo ya hivi karibuni.
Bwana Mattis amesema kuwa kombora hilo liliruka juu ikilinganishwa na kombo jingine lolote lile hapo awali.
''Korea Kaskazini ilikuwa ikiunda kombora linaloweza kuruka kutoka bara moja hadi jingine ambalo linaweza kurushwa eneo lolote lile duniani'', aliongezea.

Makombora ya Korea Kaskazini
Image captionMakombora ya Korea Kaskazini

Rais wa Marekani Donald Trump aliarifiwa kuhusu hatua hiyo wakati ambapo kombora hilo bado lilikuwa angani kulingana na Ikulu ya Whitehouse.''Tutalishughulikia''.

Comments

Popular posts from this blog

Jifunze Jinsi ya kutengeneza sabuni ya Unga na ya maji

Mkataba wa Aishi Manura wavuja ukionyesha kujiunga na simba Simba

Antoine Griezmann: Nyota wa Atletico Madrid aomba radhi baada ya kujifanya mweusi