Wavulana 2 wasafiri kilomita 80 chini ya basi China
Picha za wavulana wawili wa Kichina ambao walisafiri na basi moja kwa umbali wa kilomita 80 wakiwa chini ya gari hilo zilizua hisia kali kuhusu hali ya watoto wa taifa hilo waliowachwa nyuma.
Wawili hao ambao hawajatajwa na serikali wanatoka katika kijiji kimoja maskini Kusini mwa Guangxi na walikuwa wakijaribu kwenda kwa wazazi wao wanaofanya kazi katika mkoa jirani wa Guangdong.
Waliripotiwa kwamba wametoweka mnamo tarehe 23 Novemba na mwalimu wao na kupatikana siku hiyohiyo chini ya gari hilo katika kituo kimoja cha mabasi.
Picha na kanda za video zinaonyesha vijana hao waliojaa matope na wakining'inia chini ya basi hilo.
Kulingana na gazeti la Southern Morning (Nanguo Zaobao), wavulana hao wana umri wa kati ya miaka minane na tisa na walipatikana na maafisa wa usalama wakati basi hilo liliposimama katika kituo kimoja.
Walikuwa tayari wamesafiri katika maeneo yenye milima kwa takriban maili tatu huku wafanyikazi hao wakibaini kwamba hawakuumia.
Miili ya watoto hao ilikuwa myembamba mno hivyobasi eneo la chini la basi hilo lilikuwa eneo zuri la kujificha , mfanyikazi mmoja aliliambia gazeti hilo.
Wafanyikazi wanasema kuwa wavulana hao walikataa kuzungumza walipohojiwa.
Lakini mfanyikazi mmoja aliliambia gazeti la Southern Morning: Baadaye tulielewa kwamba wavulana hao walikuwa wakitaka kuonana na wazazi wao.
Walijificha chini ya basi hilo kwa sababu walitaka kuwaona wazazi wao.
Ripoti zinasema kuwa watu wa jamii yao waliarifiwa na vijana hao wakachukuliwa siku hiyohiyo.
Comments
Post a Comment