Hii ni nyingine mpya ya kumuenzi Robert Mugabe nchini Zimbabwe



Wiki moja baada ya kumuondoa madarakani, serikali ya Zimbabwe imetangaza siku kuu mpya ya 
kukumbuka mchango wa Robert Mugabe ambaye aliondolewa madarakani wiki iliyopita.
Gazeti la serikali la Herald limesema sikukuu hiyo itakuwa ikiadhimishwa siku ya kuzaliwa kwa Bw Mugabe kila mwaka. Uamuzi wa kusherehekea Siku ya Taifa ya Vijana ya Robert Gabriel Mugabe kila 21 Februari ulifanywa rasmi kupitia tangazo rasmi kwenye gazeti la serikali.
Tangazo hilo lilichapishwa Ijumaa – siku ambayo Rais Emmerson Mnangagwa aliapishwa kuwa rais, na kufikisha kikomo uongozi wa Mugabe wa miaka 37.
Serikali ya Bw Mugabe ilikuwa imeamua kutangaza siku ya kuzaliwa kwake kuwa sikukuu ya taifa mwezi Agosti, baada ya kampeni kutoka kwa mrengo wa vijana katika chama cha Zanu-PF.

Comments

Popular posts from this blog

GOR MAHIA MABINGWA WA SPORTPESA SUPER CUP 2017, SASA KUKIPIGA NA EVERTON JULAI 13

Marekani na Korea Kusini wafanya mazoezi ya pamoja ya jeshi

UKWELI KUHUSU MZEE MAJUTO, NA TETESI ZA KUFA