Kuapishwa kwa Uhuru Kenyatta: Usalama waimarishwa Nairobi

Wanajeshi wakijiandaa kwa sherehe ya kuapishwa kwa rais Uhuru Kenyatta katika uwanja wa michezo wa Kasarani Nairobi


Haki miliki ya pichaAFP
Image captionWanajeshi wakijiandaa kwa sherehe ya kuapishwa kwa rais Uhuru Kenyatta katika uwanja wa michezo wa Kasarani Nairobi

Usalama umeimarishwa katika mji mkuu wa Kenya Nairobi wakati wa siku ambayo rais Uhuru Kenyatta anatarajiwa kuapishwa kwa awamu ya pili ya urais.
Takriban viongozi 13 wa mataifa tofauti wanatarajiwa kuhudhuria hafla hiyo.
Kiongozi wa upinzani Raila Odinga ambaye alisusia marudio ya uchaguzi ameitisha kufanyika kwa mkutano wa upinzani licha ya mkutano huyo kupigwa marufuku.
Uchaguzi wa mwezi Agosti ulifutiliwa mbali na mahakama kutokana na kile kilitajwa kuwa uchaguzi usio huru na haki.
Marudio ya uchaguzi wa Oktoba 26 ulimpatia Uhuru Kenyatta asilimia 98 ya kura huku waliojitokeza kushiriki katika shughuli hiyo wakiwa asilimia 39.
Sherehe hiyo ya siku ya Jumanne inayofanyika katika uwanja wa michezo wa Kasarani jijini Nairobi inatarajiwa kuanza mwenzo wa saa nne.
Waandalizi wanatarajia watu 60,000 kujaza uwanja huo huku skrini kubwa zikiwa zimewekwa nje ya uwanja huo kwa wale watakaoshindwa kuingia.

Rais Kenyatta anakabiliwa na wakati mgumu wa kuliunganisha taifa hiloHaki miliki ya pichaEPA
Image captionRais Kenyatta anakabiliwa na wakati mgumu wa kuliunganisha taifa hilo
Baadhi ya watumbuizaji wanaotarajiwa kuhudhuria sherehe hiyoHaki miliki ya pichaAFP
Image captionBaadhi ya watumbuizaji wa kabila la Maasai wanaotarajiwa kuhudhuria sherehe hiyo

Naibu wa rais William Ruto, pia ataapishwa.
Miongoni mwa viongozi wa kigeni wanaotarajiwa ni waziri mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu, rais wa Uganda, Yoweri Museveni na rais wa Rwanda Paul Kagame.
Upinzani nchini humo umewataka wafuasi wake kususia sherehe hiyo na badala yake kukusanyika katika mkutano ili kuwakumbuka wafuasi waliouawa katika ghasia tangu uchaguzi wa mwezi Agosti.

Upinzani ulikabiliana na Polisi baada ya uchaguzi wa Agosti 8Haki miliki ya pichaEPA
Image captionUpinzani ulikabiliana na Polisi baada ya uchaguzi wa Agosti 8

Maafisa wapolisi wameonya upinzani huo dhidi ya kufanya mkutano huo.

Comments

Popular posts from this blog

Jifunze Jinsi ya kutengeneza sabuni ya Unga na ya maji

Mkataba wa Aishi Manura wavuja ukionyesha kujiunga na simba Simba

Antoine Griezmann: Nyota wa Atletico Madrid aomba radhi baada ya kujifanya mweusi