Posts

Video ya dakika 2 ikionyesha Hat-Trick ya Okwi iliyookoa Milioni 5

Image

Hizi Ndizo Mbinu Bora Za Kuepuka Majanga Kwenye Uwekezaji Wako Wa Majengo.

Image
Wakati tulionao sasa ni wakati bora sana wa sisi kuendelea kupeana hamasa katika kuzitumia rasilimali zetu katika kujiletea maendeleo yetu binafsi pamoja na nchi yetu kwa ujumla. Hatuna sababu zozote za kukata tamaa pale mambo yanapokuwa magumu na hakuna dalili yoyote ya wewe kusonga mbele, bali kwetu inapaswa kuwa fursa ya kutafakari upya na kuchukua hatua bora zaidi zitakazotusaidia kutimiza malengo yetu. Nidhamu na juhudi ndiyo nguzo yetu katika kufanikisha kila jambo ambalo tumeamua kulifanyia kazi. Pamoja na hayo zipo changamoto za kimazingira katika uwekezaji wa majengo ambazo zinatokana na usimamizi na mabadiliko ya kisera na kisheria ambazo si za mtu mmoja bali ni za nchi kwa ujumla. Kiini cha mabadiliko hayo ni maendeleo ya kiuchumi na uboreshaji wa mazingira katika kuifanya nchi yetu kuwa mahali bora na salama kwa kila mmoja wetu.  Mabadiliko haya yanawaathiri baadhi ya marafiki zetu ambao wamejikuta wakiguswa kwa namna tofauti. Njia pekee katika kutatua ch...

Tanzania yakataa wakimbizi wa Burundi nchini humo

Image
Image caption Wakimbizi wa Burundi walioingia Tanzania Serikali ya Tanzania imelipatia shirika la wakimbizi duniani UNHCR siku saba kuanza kuwarudisha wakimbizi wa Burundi ambao wanataka kurudi kwao kwa hiari, ama sivyo serikali yenyewe itafanya zoezi hilo yenyewe. Waziri wa mambo ya ndani wa Tanzania Mwigulu Nchemba ametoa agizo hilo siku ya Alhamisi alipokuwa katika ziara ya kikazi katika kambi ya Nduta Magharibi mwa Tanzania ambayo ni moja ya kambi zinazohifadhi wakimbizi wengi wa Burundi. Tanzania ndio nchi inayoongoza Afrika Mashariki kwa kuhifadhi wakimbizi wengi kutoka Burundi. Bwana Nchemba amewashutumu maafisa wa UNHCR kwa kuchelewesha zoezi hilo la kuwarudisha nyumbani wakimbizi wa Burundi wanaotaka kurejea nchini kwao kwa hiari. Enable it in your browser or pata Flash Player hapa. Samahani, unahitaji Flash kucheza taarifa hii Tanzania yatahadharisha wahalifu waliotoka Burundi Zaidi ya wakimbizi elfu 8 kati ya laki moja ishirini...

UN yataka mapigano kusitishwa Syria kupisha misaada

Image
Image caption Raia wengi wapo katika hali mbaya kwa kukosa chakula na huduma nyingine muhimu Umoja wa Mataifa umetoa wito kusimamishwa kwa muda mapigano katika mji wa Ragga nchini Syria, kuruhusu idadi ya raia waliopo katika eneo hilo la mapigano kuondoka. Mkuu wa misaada ya kibinadamu nchini Syria, Jan Egeland, anasema mji wa Raqqa yawezekana kwa sasa ni moja kati maeneo hatari duniani na kutaka hatua za haraka kuchukuliwa ili kutoa mwanya kwa raia kutoroka katika eneo hilo. Amesema kuwa wapiganaji wa Islamic State wanatumia kundi la raia waliobaki kama kinga ya kivita. Hata hivyo idadi hiyo ya raia wapatao 25,000 kwa wamekwama ndani ya mji huo huku kukiwa na mfululizo wa mashambulizi ya anga kwa juma moja lililopita. Image caption Ragga unatajwa kuwa miongoni mwa miji hatari zaidi duniani Shirika la kimataifa la Amnesty linasema mamia ya watu wameuawa tangua mashambulizi hayo yalipoanza katika mji wa Raqqa mwezi june mwaka huu. Wapiganaji wa IS wanatuhumiwa na umoja...

Everton waingia hatua ya makundi Europa League

Image
Haki miliki ya picha Image caption Sigurdsson alifunga bao mechi yake ya kwanza aliyokuwa kwenye kikosi cha kuanza mechi Ulaya tangu Machi 2014. Gylfi Sigurdsson alianza mechi yake ya kwanza Everton kwa kufunga bao akiwa hatua 50 kutoka kwenye goli na kusaidia vijana hao wa Ronald Koeman kufika hatua ya makundi katika ligi ndogo ya klabu Ulaya, Europa League. Everton walitoka sare ya 1-1 ugenini mechi hiyo dhidi ya Hajduk Split ya Croatia lakini wakasonga kwa ushindi wa jumla wa 3-1. Klabu hiyo ya England ilikuwa ikiongoza 2-0 kutoka kwa matokeo ya mechi ya kwanza na matumaini yao yalionekana kukaribia kufutika baada ya Josip Radosevic kumbwaga kipa Jordan Pickford. Lakini Sigurdsson, aliyekuwa akichezea Everton mara yake ya pili tangu wamnunue £45m kutoka Swansea alisawazisha sekunde 14 baada ya kuanza kwa kipindi cha pili. Bao la Sigurdsson liliwaacha Hajduk wakihitaji kufunga mabao matatu ndipo wafanikiwe kusonga. Wayne Rooney, aliyekuwa kwenye kikosi cha kuanza mec...

Yingluck: Mahakama yatoa kibali waziri mkuu wa zamani Thailand akamatwe

Image
Haki miliki ya pich Image caption Mamia ya wafuasi wa Bi Yingluck walifika nje ya majengo ya mahakama ya juu Bangkok Mahakama ya Juu nchini Thailand imeahirisha kikao cha kutoa hukumu katika kesi ambapo waziri mkuu wa zamani wa nchi hiyo Yingluck Shinawatra ameshtakiwa makosa ya uhalifu ya kuzembea kazini. Majaji hao wakiwa mjini Bangkok wametoa kibali cha kukamatwa kwake wakisema hawaamini alivyosema kwamba amekosa kufika mahakamani kwa sababu anaugua. Mahakama imeahidi kutoa huku tarehe 27 Septemba. Ijumaa, mawakili wa Bi Yingluck waliomba hukumu icheleweshwe na kuambia mahakama kwamba anaugua ugonjwa wa vertigo na hawangeweza kufika kortini. Lakini taarifa rasmi ya Mahakama ya Juu imesema waendesha mashtaka "hawaamini mshtakiwa ni mgonjwa kwani hakuna cheti chochote cha matibabu kilichowasilishwa kwa mahakama, na kwamba hali yake ya afya si mbaya mno kiasi kwamba hawezi kufika kortini." Mahakama imesema itatoa kibali cha kukamatwa kwake kwani anaweza kuiki...

Taarifa muhimu kwa wote walioomba na watakaoomba kazi Serikalini

Image
Mtakumbuka Serikali katika mwaka wa fedha uliomalizika  2016/2017  iliahidi kutoa Ajira serikalini zaidi ya  52,000  kwa Watanzania, ambapo katika siku za hivi karibuni Serikali imekuwa ikitoa vibali vya kuajiriwa watumishi wa kada mbalimbali ikiwemo Waalimu wa Sayansi, Kada za Afya na maeneo mengine kulingana na mahitaji. Kama mnavyofahamu mojawapo ya jukumu la msingi la kuanzishwa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma ni pamoja na kuendesha mchakato wa ajira kwa niaba ya waajiri mbalimbali na hatimae kuwapangia vituo vya kazi waombaji kazi wanaofaulu usaili, ambapo tangu Serikali ilipoanza kutoa vibali baada ya kusitishwa tumeshapokea jumla ya vibali kwa ajili ya mamlaka za Ajira  239,  kati ya hivyo vipo ambavyo vimeshafanyiwa kazi na vingine mchakato wake unaendelea katika hatua mbalimbali. Aidha, baadhi ya vibali ambavyo mchakato wake umeshakamilika ni pamoja na  kibali cha Mamlaka ya Chakula na Dawa  (TFDA) ...