Posts

Riyad Mahrez kukamilisha uhamisho wake, anaelekea wapi?

Image
Haki miliki ya picha TWITTER Image caption Riyadh Mahrez kuondoka Leicester Riyad Mahrez ameruhusiwa kuondoka katika kambi ya kikosi cha Algeria na kurudi Ulaya ili kukamilisha uhamisho wake hadi klabu mpya kulingana na shirikisho la soka nchini Algeria. Winga huyo wa Leicester aliwasilisha ombi la kutaka kuondoka katika uwanja wa King Power na amehusishwa na vilabu vingi huku Roma ikiwa tayari imewasilisha ombi la kumununua mchezaji huyo mara tatu , ombi la mwisho likiwa lile la dau la £32m. Klabu kama vile Barcelona, Arsenal, Manchester United na Chelsea zimeripotiwa kutaka kumsajili Mahrez ambaye alikuwa mchezaji bora 2016 baada ya kuwa kiungo muhimu wa timu ya Leicester ilioshinda kombe la ligi ya Uingereza msimu huo.

Kaka wa Salman kupanda kizimbani Libya

Image
Haki miliki ya picha LIBYA INTERIOL MINISTERY Image caption Hashem Abedi Maafisa nchini Libya wamesema Hashem Abedi, kaka wa mshambuliaji wa bomu la kujitoa mhanga, lililouwa watu 22 katika mji wa Manchester, Uingereza atafikishwa mahakamani mjini Tripoli kwa kuhusika na shambulio hilo. Hashem Abeid aliyekuwa na miaka 20 alikamatwa mjini Tripoli muda mfupi baada ya mlipuko huo wa Manchester. Mkurugenzi wa upelelezi katika kesi hiyo nchini Libya, Sadiq Al Sour ameiambia BBC kwamba dalili zote zinaonesha mshtakiwa huyo ndiye aliyemsaidia mdogo wake Salman. Baba yao ambaye pia alikamatwa, ameachiwa kutoka rumande.

Marekani: Tutaendelea na mazungumzo na Korea Kaskazini

Image
Image caption Rais wa Korea Kaskazini Kim Jong-un na mwenzake wa Marekani Donald Trump Waziri wa ulinzi nchini Marekani James Mattis amesema kuwa Marekani itaendelea na mazungumzo ya kidiplomasia na Korea Kaskazini. Matamshi hayo yanajiri baada ya rais Donald Trump kusema katika mtandao wake wa Twitter kwamba mazungumzo sio suluhu kwa mipango ya kijeshi ya Korea Kaskazini. Urusi pia imeionya Marekani dhidi ya kuchukua hatua za kijeshi akisema madhara yake yatakuwa makubwa. Korea Kaskazini ilizuwa wasiwasi baada ya kurusha kombora kupitia anga ya Japan siku ya Jumanne. Kombora hilo ambalo Japan limelitaja kuwa tishio lisilo la kawaida , lilivuka katika anga ya kaskazini ya kisiwa cha Japana cha Hokkaido mapema siku ya Jumanne, na kusababisha raia kujificha kabla ya kombora hilo kuanguka baharini yapata kilomita 1,180 . Korea Kaskzini baadaye ilisema kuwa ni hatua mojawapo ya operesheni zake za kijeshi katika eneo la pacific na kurejelea tishio lake la kushambulia kisiwa...

Wafikishwa mahakamani Uganda kwa mauaji

Image
Haki miliki ya picha UGANDA POLICE Image caption Polisi nchini Uganda Watu 12 wamefikishwa mahakamani nchini Uganda kwa mashtaka ya mauaji ya wanawake tisa katika eneo la kaskazini nje ya mji mkuu Kampala. Kati ya washtakiwa hao wawili ni wanawake. Wote kwa pamoja wanashtakiwa kwa makosa ya ugaidi na wizi wa kutumia nguvu. Jumla ya wanawake 19 wameuawa katika maeneo ya mji wa Kampala tangu mwezi Mei. Wengi kati yao walikuwa wamebakwa na kukatwa viungo vyao, huku miili yao ikiachwa porini na pembezoni mwa barabara. Mkuu wa polisi nchini Uganda amesema imani za kishirikina zinahusishwa katika baadhi ya mauaji.

Tetesi za Soka Ulaya Jumatano 30.08.2017

Image
Haki miliki ya picha GETTY IMAGES Tottenham wanakaribia kukamilisha usajili wa beki wa kimataifa wa Argentina Juan Foyth, 19, kutoka Estudiantes kwa pauni milioni 8 na pia bado wanajaribu kumsajili beki wa PSG Serge Aurier, 24, kwa pauni milioni 23. (Guardian) Liverpool wamekubali kumuuza kiungo Philippe Coutinho, 25, kwenda Barcelona kwa pauni milioni 148. (Yahoo Sports) Jose Mourinho anataka kumsajili winga wa Leicester City Riyad Mahrez. (SFR Sport) Arsenal huenda wakashawishiwa kumuuza Alexis Sanchez, 28, iwapo watapata dau la kuvutia. (BBC Radio 5 live) Arsenal wamekataa dau la pauni milioni 30 kutoka Liverpool la kumtaka Alex Oxlade-Chamberlain, ambaye pia amekataa kwenda Chelsea kwa pauni milioni 40. (Evening Standard) Haki miliki ya picha REUTERS Raheem Sterling atabakia Manchester City na hatokuwa sehemu ya mkataba wa City kumsajili Alexis Sanchez kutoka Arsenal. (Sky) Sergio Aguero huenda akataka kuondoka Manchester City mwezi Januari iwapo Pep Guardiola a...

Liverpool waanza mazungumzo kuhusu Oxlade-Chamberlain Sambaza habari hii Email

Image
Haki miliki ya picha GETTY IMAGES Image caption Alex Oxlade-Chamberlain alianza kwenye mechi ambayo Arsenal walishindwa Anfield Jumapili Liverpool wameanza mazungumzo na Arsenal kuhusu uhamisho wa kiungo wa kati Alex Oxlade-Chamberlain. Mchezaji huyo wa miaka 24 alikataa kuhamia Chelsea Jumanne hata baada ya klabu hizo kuafikiana kuhusu uhamisho wake wa £40m. Oxlade-Chamberlain anayechezea timu ya taifa ya England anataka kucheza kama kiungo katika safu ya kati na anahisi kwamba anaweza akapata nafasi Anfield. Alikataa kuhamia Chelsea baada ya kugundua kwamba huenda wakataka kumtumia katika upande wa kushoto uwanjani. Bado haijabainika iwapo Liverpool watafikia dau ambayo Chelsea walikuwa wamewasilisha. Oxlade-Chamberlain anatumikia mkataba wake wa mwisho Emirates na amechezea mechi zote nne za Arsenal msimu huu licha yake kumwambia meneja Arsene Wenger kwamba hatatia saini mkataba mpya. Alishangiliwa na wachezaji wa Liverpool alipoondolewa uwanjani wakati wa mechi...

Chuo chatuma dola milioni moja kwa mwanafunzi kimakosa Afrika Kusini

Image
Haki miliki ya picha WSU/TWITTER Image caption Chuo Kikuu cha Walter Sisulu Chuo Kikuu kimoja nchini Afrika Kusini kimesema kwamba kilituma kimakosa jumla ya randi milioni 14 ambazo ni sawa na dola milioni moja za Marekani katika akaunti ya benki ya mwanafunzi mmoja nchini humo. Pesa hizo zilitoka kwenye mfuko wa shirika la kufadhili wanafunzi kimasomo nchini humo NSFAS. Chuo Kikuu cha Walter Sisulu, kinasema kuwa pesa hizo ziliwekwa miezi mitano iliyopita, huku makosa hayo yakijulikana baada ya risiti ya akaunti ya mwanafunzi huyo kuonyesha kuwa na mamilioni ya pesa baada ya kuwekwa katika mtandao wa kijamii. Chuo hicho kikuu sasa kinachunguza ni kwa nini mwanafunzi huyo hakupiga ripoti ya kuwepo kiasi kikubwa hivyo cha pesa kwenye akaunti yake. Mwanafunzi huyo amekanusha madai hayo.  Ripoti ya shirika la habari la EWN inasema picha zimeonekana kwenye mitandao ya kijamii, zikionyesha mwanafunzi huyo wa kike huyo akijisifu na kujionyesha kwenye sherehe moja h...