Posts

Showing posts from June, 2015

VIDONDA VYA TUMBO.

Image
  VIDONDA VYA TUMBO,DALILI NA MATIBABU YAKE Imekuwa ni changamoto sana kwa watu wanaosumbuliwa na vidonda vya tumbo hii ni kwa sabubu zifuatazo 1.        Jamii haijatambua kuwa vidonda vya tumbo husababishwa na mienendo ya maisha yetu. Hivyo tiba yake kuu ni kubadili maisha tunayoishi nayo,kuanza lishe tunayopata,jamii tunayo ishi nayo, na kuepuka vinywaji vinavyo hatarisha afya ya ukuta wa mfuko wa chakula. 2.        Dawa kama omeprazole na zingine nyingi ambazo kwa pamoja tunaziita PROTON PUMP INHIBITORS zinapunguza utoaji wa asiodi ambayo ikitolewa kwa wingi inaenda kuharibu kuta za mfuko wa chakula. Hivyo zinazuia tu tindikali bila kushugulika na chanzo cha kuongezeka kwa hiyo tindikali. Hivyo bila kuondoa chanzo kinachosababisha kuongezeka kwa tindikali hiyo ya HCL hata siku moja huwezi kupona ndio mana siku hizi kuna dawa za kutuliza kama mmoja wapo wa wagonjwa nilikutana nae anasema hivyo. Inaweza kuwa leo...
Image
WASANII BARNABA NA V.MONEY VANESA Hatimae Aliyekuwa Akitegemewa Kupata Tuzo ya Mtunzi Bora wa Mwaka Kill Awards Mwanamuziki Barnaba Ametoa ya Moyoni Baada ya Kuikosa Tuzo Hiyo: Barnaba - Nawashukuru watu wangu wote na mashabiki Zangu mlionipiga Kura naamini kila kilichotokea Kimestahiri Kutokana Mimi nampenda mungu na naamini kuna Kitu kinaitwa Wakati au muda na napenda Changamoto mana hii Itafanya Nifanye Vyema mara mbili ya pale ninapofanyaga Yes Of coz mimi sinaga Team Bali Team yangu ni wale wote wanaopenda Muziki Mzuri nawapenda wote na nawapa Ongera wenzangu wote mlioshinda Bila kusahau kipenzi Changu #bestfemaleperformer and #bestfemaleartist @Vanessamdee Kushinda kwako ni wazi inaonesha wazi kazi nzuri Aya Tunaendelea na kazi Ya kuangusha Vyuma Juu Ya Vyuma na mwaka Huu natoa #Album Ambayo itafanya Yule asiyemwelewa Barnaba ajue na aelewe mwisho nawakumbusha Umoja ni nguvu utengano............. Tusijenge Matabaka Nndugu zangu

MTOTO WA AFRIKA.

Image
MAADHIMISHO YA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA-                                    JUNI 16,2015 JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO MAELEZO YA KATIBU MKUU KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU MAADHIMISHO YA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA ITAKAYOADHIMISHWA TAREHE 16 JUNI, 2015 Utangulizi: Tarehe 16 Juni ya kila mwaka Tanzania huungana na Nchi nyingine za Afrika kuadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika. Mnamo mwaka 1990, uliokuwa Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU) ulipitisha Azimio la kuwakumbuka watoto wa kitongoji cha Soweto kilichopo Afrika ya Kusini waliouawa kinyama na iliyokuwa Serikali ya Makaburu ya nchi hiyo tarehe 16 Juni, 1976. Watoto hao walikuwa wakidai haki ya kutobaguliwa na haki nyingine za kibinadamu. Hivyo, OAU iliazimia kuwa tarehe 16 Juni ya ki...

Kikombe kimoja cha kahawa kwa siku chapunguza hatari ya ugonjwa wa moyo

Image
Mbali na faida kemkem tunazozijua zinazopatikana kwenye kahawa, utafiti mpya umesema kwamba kunywa kikombe kimoja tu cha kahawa kwa siku kunapunguza hatari ya kupatwa na mshituko wa moyo. Utafiti huo uliotolewa katika Kongamano la Jumuiya ya Mshituko wa Moyo la Kimataifa nchini Marekani, umeeleza kwamba kunywa kikombe kimoja cha kahawa ya kawaida na isiyokuwa na kafeini kila siku huzuia kupatwa na mshituko wa moyo kwa asilimia 30. Hata hivyo wataalamu wameonya kuwa kutumia sana kinywaji hicho matokeo yake huweza kuwa kinyume. Tafiti za huko nyuma pia zilionyesha kuwa, kunywa kila siku kahawa kunaweza kumzuia mtu asipate kisukari aina ya pili na ugonjwa wa akili. Mpenzi mdau baada ya kufahamu hayo, nimeonea nichukue fursa hii kuelezea baadhi ya faida za kahawa. Mbali ya kawaha kuwa kinywaji murua ambacho kinaweza kukufanya uchangamke asubuhi baada ya kuamka, au kwa wale kina yakhe wanaopenda kuburudika kwa kunywa kahawa kwa kashata vijiweni au kando ya barabara huk...

ZIJUE FAIDA ZA MBEGU ZA MABOGA

Image
Mandai Herbalist Clinic hapa inakufahamisha baadhi ya faida za mbegu za maboga, lakini kwanza ni vizuri ifahamike kuwa mbegu za maboga hutokana na tunda liitwalo boga, tunda ambalo asili yake haifahamiki vizuri ni wapi, ingawaje baadhi ya tafiti zinasema kuwa asili yake ni Amerika ya kaskazini. Zao la maboga mara nyingi hushamiri zaidi katika msimu wa joto na inashauriwa kupanda zao hili mwanzoni mwa mwezi Julai hasa katika udongo unaotunza maji vizuri. Hata hivyo zao hili huweza kuathirika endapo kutakuwa na upungufu wa maji au joto dogo sana, lakini pia zao hili huweza kuathirika linapopandwa katika udongo ambao hauchuji maji vizuri. Lakini tukiachana na hayo ni vizuri ifahamike kwamba mbegu za maboga zinafaida nyingi sana kiafya na hujumuisha kiwango kingi cha protini na vitamin, huku ikiaminika kwamba, mbegu hizo huweza kupunguza mafuta kwenye mishipa ya damu na jambo la msingi zaidi ni kwamba gramu moja ya mbegu za maboga huwa na protini sawa na glasi moja ...

JITIBU MAGONJWA 27 KWA ASALI NA MDALASINI

Image
Mdalasini  Asali                          MDALASINI NA ASALI Taswira  ya  mtu  anayesumbuliwa  na  tatizo  la  chunusi  ambalo  linaweza  kuondoka  kwa  kutumia  mdalasini  kama  makala  haya  yanavyo  elekeza.  " MDALASINI NA ASALI vinaweza kukufanya uonekane kama picha yenye afya nzuri kama ile ya mwonyeshaji mitindo ya mavazi na muigizaji sinema Jocqol Bell." Asali inafahamika vema Duniani kote kama mojawapo ya silaha ya kiajabu katika kupigana na magonjwa na matatizo yatokanayo na uzee. Sasa hivi, utafiti mpya umeonyesha kwamba uwezo wa asali unaweza kuongezwa maradufu kama itachanganywa na mdalasini wa kawaida. Uchunguzi wa kina ufanywao kwa wiki na jarida la World News wa Tiba, wataalamu wa madawa yatokanayo na mimea pamoja na kijarida ...

BAMIA INAWEZA KUTIBU TATIZO LA KISUKARI

Image
Wanasayansi   nchini   Marekani    wamegundua   kuwa   Bamia   ina   virutibisho   vinavyo   weza   kumsaidia mtu   mwenye   tatizo   la   Sukari.                              JINSI     YA   KUTUMIA   : Chukua   bamia   zako   kisha   kata   vichwa   vyake   , halafu   ziloweke   bamia     kwenye   kikombe   cha   maji   kwa   usiku   mzima   kisha   zitoe   bamia   halafu   kunywa   maji   yako. Fanya   hivyo   kwa   muda   wa   siku   ishirini   na   moja   na   kwa   uwezo   wa   Mungu,   tatizo   la   sukari   litakwisha. ...

WATU SITA MBARONI KWA KUKUTWA NA MIFUPA 6 YA WATU.

Image
JESHI la Polisi mkoani Tabora, limewakamata na kuwafikisha mahakamani watu sita, kwa tuhuma za kukutwa na mifupa sita ya binadamu, inayodhaniwa kuwa ni ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albino). Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Suzan Kaganda alisema watuhumiwa hao walikamatwa asubuhi ya Mei 22, mwaka huu wilayani Igunga. Kaganda aliwataja watuhumiwa hao wanaodaiwa kukiri kujihusisha na matukio ya kudhuru albino kuchukua viungo kuwa ni Mussa Njile (30), mkazi wa Mnale, Elizabet Masanja (42), mkazi wa Bungwa. Wengine ni Bahati Kilungu (56), ambaye ni mwalimu na mkazi wa Mbutu Kahama, Bilia Masanja (38), mkazi wa Bukene wilayani Nzega, Muhoja John (28), mkazi wa Nyasa na Rejina Kashidye (40), mkazi wa Isegenhe. Kamanda Kaganda alikumbushia tukio la Agosti 16, mwaka jana, katika kitongoji cha Mikese kijiji cha Buhelela wilayani Igunga mkoani hapa la kuuawa kwa Mapambo Mashiri aliyekuwa amelala nyumbani kwake na mkewe, Mungu Masanja, mwen...

January makamba achukua fomu ya ugombea urahisi.

Image
Mbunge  wa jimbo la Bumbuli, mjumbe wa NEC na Naibu Waziri wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba baada ya kutangaza nia  jana juni 10, amechukua fomu  katika Ofisi Kuu za Chama Cha Mapinduzi mjni Dodoma  ya kuomba kuteuliwa kugombea urais kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi. Akizungumza mara baada ya kuchukua fomu Makmba alisema kwamba ataendelea na safari yake  nchi nzima kutafuta wadhamini  ambao ni  wanachama wa CCM ikiwa ni sehemu ya hitaji la chama kuwa na wadhamini 450. Hata hivyo  aliwashukuru  wananchi kwa  kuungana naye  kutoka katika kila kona ya nchi  na nje ya nchi huku akisisitiza kuwa  ni zama mpya, za kizazi kipya kuamua na kujenga kesho ya nchi yetu
Image
MASWALI YALIYOWAKIMBIZA WATANGAZA NIA URAIS NDANI YA CCM YAWEKWA HADHARANI   Edward Lowassa ni mmoja wa wagombea urais kupitia CCM.   Dar es Salaam. Siku moja baada ya kuahirishwa kwa mdahalo wa waliotangaza nia katika nafasi ya urais CCM, imebainika kuwa viongozi hao wangepaswa kujibu maswali magumu manane yanayohusu uchumi, utawala bora na utawala wa sheria. Hata hivyo mgombea Balozi Amina Salum Ali pekee ndiye aliyejitokeza.  Baadhi ya wagombea waliokuwa wametajwa kuhudhuria mdahalo huo wa moja kwa moja kupitia televisheni ni Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba, Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba, Waziri Mkuu mstaafu, Fredrick Sumaye na Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu na Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta. Akizungumzia utaratibu wa mdahalo huo ulioandaliwa na Umoja wa Maofisa Watendaji Wakuu wa Kampuni Binafsi nchini ( CEOrt), Mwenyekiti wake Ali Mufuruki alisema, kila mtangaza nia alitakiwa ...
Image
Madhara ya kuvuta sigara Mwili wa mvutaji sigara ulivyo adhiriwa. Kila sekunde nane, mtu mmoja hufariki kutokana na utumizi wa  tumbako . Imebainika kuwa saba kati ya wavutaji sigara kumi, huanza  uraibu  huu wakiwa wangali watoto. Wanaoendelea kuvuta sigara kwa muda mrefu hufupisha maisha yao kwa miaka 20 hadi 25. Sababu ni kuwa sigara ina kemikali zaidi ya 4,000 ambazo zina uwezo wa kudhhuru afya ya binadamu. Madhara yanayosababishwa na uvutaji sigara ni mengi na yamesambaa mwilini kote. Yafuatayo ni baadhi tu ya maradhi yatokanayo na utumiaji wa tumbako. Yaliyomo    [ ficha ]  1   1.Kung’oka kwa nywele 2   2.Magonjwa ya macho 3   3.Kukunjana kwa ngozi 4   4.Magonjwa ya masikio 5   5.Saratani ya ngozi 6   6.Magonjwa ya meno 7   7.Magonjwa ya mapafu 8   8.Mifupa 9   9.Ugonjwa wa moyo 10   10.Vidonda vya tumboni 11   11.Vidole 12   12.Wanawake 13   13.Wana...