Basel yaichapa Benfica 5-0 Uefa
Michuano ya kuwania taji la Klabu Bingwa Barani Ulaya (Uefa champions Ligi) imechezwa usiku wa kuamkia leo Alhamisi katika hatua ya makundi kwa michezo mbalimbali.
Kundi A- FC Basel wakiwa nyumbani wameibugiza Benfica 5-0, CSKA Moscow wakiwa nyumbani walikubali kipigo cha mabao 4 -1 na Manchester United huku Romelu Lukaku akifunga mara mbili, Martial na Mkhtaryan walifunga bao moja moja huku bao la Moscow likifungwa na Kuachev na kuwafanya United kuongoza kundi A.
Kundi B - Psg wakiwa nyumbani wameshinda mabao 3-0 dhidi ya Buyen Munich ambapo wachezaji Dani Alves, Neyamar na Edison Cavanni wamefanikiwa kuifunga Bayern Munich bao 3 huku Celtic wakiwa ugenini wakiifunga Anderchelt mabao 3 mabao ya Celtic yakiwekwa kimiani na Patrick Roberts, Scott Sinclair na Griffiths.
Kundi C FC Qarabag imechapwa 2-1 na AS Roma, Atletico Madrid imefungwa 2-1 dhidi ya Chelsea. Kundi D- Gonzalo Higuain na Mario Mandzukic waliisaidia Juventus kupata alama 3 baada ya kupata ushindi dhidi ya Olympiacos wa mabao 2-0, huku Barcelona wakizidi kujichimbia ugenini baada ya goli la kujifunga Sporting la Sebastian Coates.
Comments
Post a Comment