Mmiliki wa Facebook apinga kauli ya Trump kuwa wanampinga

facebook


Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMkuu na mwanzilishi wa mtandao wa Facebook ,Mark Zuckerberg

Mkuu na mwanzilishi wa mtandao wa Facebook ,Mark Zuckerberg, amebeza maoni ya rais Donald Trump dhidi ya mtandao huo kwamba umekuwa ukimpinga.
Zuckerberg amesema pande zote mbili za kisiasa nchini Marekani zilikuwa zikiutazama mtandao wa Facebook tofauti kutokana na kutofurahishwa na maoni yanayotolewa na watumiaji.
Ameongeza wakati wa uchaguzi Democrats wamewahi tuhumu mtandao huo kwamba unamsaidia Trump.
Mwanzilishi huyo wa Facebook amebainisha kuwa wakati wote wa uchaguzi mtandao wake ulifanya unachoweza kwa manufaa ya wapiga kura.
Hivi punde Facebook itawasilisha matangazo ya kisiasa 3,000 kwa wachunguzi wa serikali wanaochunguza tuhuma za Urusi kuingilia uchaguzi mkuu wa Marekani.
Mtandao huo unaamini huenda matangazo hayo yalinunuliwa na mashirika ya Urusi wakati na baada ya uchaguzi huo wa urais 2016.
Facebook, Twitter na Google imeombwa kutoa ushahidi mbele ya kamati ya kijasusi ya bungela seneti Marekani Novemba 1 kuhusu tuhuma za Urusi kuwa na mkono katika uchaguzi wa Marekani.
Facebook na Google zimethibitisha zimepokea mualiko kuhudhuria kikao cha kamati hiyo, lakini hakuna katika mitandao hiyo iliyothibitisha kuwa itahudhuria.

Comments

Popular posts from this blog

Jifunze Jinsi ya kutengeneza sabuni ya Unga na ya maji

Mkataba wa Aishi Manura wavuja ukionyesha kujiunga na simba Simba

Antoine Griezmann: Nyota wa Atletico Madrid aomba radhi baada ya kujifanya mweusi