Brigthon yaizamisha Newcastlle United EPL
Klabu ya soka ya Brigthon Hove Albion jana Jumapili ikimenyana na Newcastlle United ilifanikiwa kapata alama tatu baada ya kuchomoza na ushindi wa bao 1-0 kwa bao la Tomer Hemed la dakika ya 51 kipindi cha kwanza na kufikisha alama 7 katika msimamo.
Kwa matokeo hayo sasa nafasi tano bora za juu katika msimamo wa ligi ya England Manchester city ni vinara sawa na Manchester United kwa usawa wa alama 16 ikiwa ni utofauti wa magoli ya kugunga na kufungwa, Chelsea ipo nafasi ya tatu,Tottenham nafasi ya nne na Liverpool ipo nafasi ya tano. Westham United, A.F.C Bournemouth na Crystal Palace zinaburuza mkia
Ligi hiyo inatarajiwa kuendelea tena leo jumatatu kwa mchezo mmoja pekee ambapo Arsenal watakuwa wakimenyana na West Brom Wich Albion katika dimba la Emirates.
Comments
Post a Comment