Uchaguzi Ujerumani: Ushindi usio wa kishindo kwa Merkel
Angela Merkel anaonekana amechoka, alipowasili katika makao makuu ya chama chake baada ya kumalizika uchaguzi.
Akitoka katika gari lake alitabasamu kwanza kwa wapiga picha waliomsubiri alafu kwa wafuasi wa chama chake waliokusanyika katika makao ya chama cha CDU.
Kansela alitambua kwamba huenda angeshinda uchaguzi huu. Lakini sio ushindi alioutarajia yeye binfasi wala chama chake. Ni matokeo mabaya kwa chama hicho cha kihafidhina chini ya utawala wake.
Huenda ni matokeo ya uamuzi wake kuwafungulia mlango mamilioni ya wakimbizi kuingia Ujerumani.
Akihotubia wafuasi wa chama chake, Bi Merkel amekiri kwamba miaka minne iliyopita imekuwa migumu. Licha ya hayo chama chake kimefanikiwa kwa lengo lake - Kuibuka mshindi.
Nderemo hazikuwa kubwa kwasababau ushindi mkuu wa uchaguzi huu ni wa AfD.
Upande wa pili wa mji huo, katika chumba kilicho sheheni vibofu vya rangi ya samawati na nyeupe, wafuasi wa chama kinachopinga uhamiaji, kinachopinga Umoja wa Ulaya walisherehekea ilipobainika
kwamba hawatoingia bunge kwa mara ya kwanza tu, lakini kwamba watakuwa wafuasi wa chama cha tatu kwa ukubwa bungeni baada ya chama cha Merkel CDU na wapinzani wake wa karibu Social democratic - SPD.
Lakini kampeni ya ubaguzi ya AfD na ghasia zilizo tatiza mikutano ya Merkel huenda ni mfano wa yanatorajiwa. Nje ya makao ya chama hicho, maafisa wa polisi wana watazama kwa makini waandamanaji
wanaokipinga AfD dhidi ya kile wengi wanaona ni maendeleo ya kushtusha ya kisiasa.
Kuna migawanyiko, na hisia ya kutoridhia katika taifa hili. Baadhi wanatishiwa na wanachokitaja kuwa ni kukuwa kwa siasa za utaifa za mrengo wa kulia.
Bi Merkel sasa ni lazima atafuta washirika wa kuunda serikali ya muungano. Na ni lazima aishawishi nchi yake na pengine baadhi ndani ya chama chake, kwamba anastahili kazi hiyo.
Zimekuwa ni kampeni ndefu na za kutia uchungu. Huenda Merkel ameshinda lakini ushindi wake hauna kishindo
Uchaguzi huu utaingia katika vitabu vya historia kwa sababu mbili. Huenda Angela Merkel ameshinda hatamu ya nne uongozini lakini ni matokeo mabaya kuwahi kushuhudiwa kwa chama chake.
Na pili wanasiasa wa mrengo wa kulia wanaoshinikiza utaifa, sasa wamejiunga katika utawala wa Ujerumani.
Kilicho kawaida ya siasa katika nchi nyingine nyingi Ulaya kilichodhaniwa hakiwezi kufanyika katika Ujerumani ya baada ya vita vikuu. Sasa kimekuwa.
Comments
Post a Comment