Kurdistan yapiga kura ya uhuru Iraq

Wafuasi huko Irbil walikusanyika kwa idadi kubwa Ijumaa


Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionWafuasi huko Irbil walikusanyika kwa idadi kubwa Ijumaa

Watu wa jimbo la Kurdistan nchini Iraq, wanashiriki kura ya maoni kuhusu uhuru wa eneo hilo licha ya pingamizi kutoka Baghdad, mataifa jirani na jamii ya kimataifa. 
Wengi wanahofia kura hiyo itachochea upya vurugu katika taifa hilo ambalo linakabiliwa na changamoto za kiusalama kutoka kwa makundi ya itikadi kali.
Kiongozi wa jimbo hilo Masoud Barzani,anasema uhuru wa eneo hilo ndio njia pekee ya kuwahakikishia usalama wakurdi.
Bwana Barzani ameongeza kuwa hatua hiyo haitaweka mpaka kati ya eneo hilo na Iraq na kwamba mazungumzo na Baghadad yataendelea kwa muda wa mwaka mmoja hadi miwili.
Kuna hofu kura hiyo ya maoni huenda ikasambaratisha Iraq na kuchochea upya mzozo kati yake na eneo hilo ambalo linasemakana halijapata uthabiti wa kisiasa.
Jamii ya kimataifa inahoji kuwa kura ya maoni inayoandaliwa leo katika eneo hilo huenda ikarudisha nyuma juhudi za kukabiliana na wanamgambo wa Islamic State nchini Iraq.
Madai ambayo maafisa wa Kurdistan wanapinga.
Iraq imeghadhabishwa na hatua hiyo na Rais wake, Haider Al Abadi, amesema serikali itachukuwa hatua madhubuti kulinda umoja wa taifa hilo.

Comments

Popular posts from this blog

Jifunze Jinsi ya kutengeneza sabuni ya Unga na ya maji

Mkataba wa Aishi Manura wavuja ukionyesha kujiunga na simba Simba

Antoine Griezmann: Nyota wa Atletico Madrid aomba radhi baada ya kujifanya mweusi