Chelsea, Man United, Man City na Tottenham zawika

Alvaro Morata alifungia Chelsea mabao matatu dhidi ya Stoke City


Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionAlvaro Morata alifungia Chelsea mabao matatu dhidi ya Stoke City

Hat-trick ya Alvaro Morata imeisaidia Chelsea kuicharaza Stoke City na kuongeza rekodi ya ushindi wao msimu huu.
Kikosi cha Antonio Conte kilichukua uongozi baada ya dakika mbili pekee, huku Morata akionyesha umahiri wake kwa kufunga krosi ya Cesar Azpilicueta na kumwacha kipa Jack Butland bila jibu.
Stoke iliizawadi Chelsea bao la pili wakati nahodha Darren Fletcher aliyempatia pasi mbaya kipa kabla ya Pedro kuingilia kati na kucheka na wavu.
Mshambuliaji Alvaro Morata alifunga bao la tatu baada ya kutamba na mipira akiwa amesalia na nusu ya uwanja kabla ya kuongeza bao lake la tatu na la nne maguu sita ndani ya eneo hatari.
Ilikuwa mchezo mzuri kwa Chelsea ambao walifunga mashambulio yao yote.
Wakati huohuo viongozi wa ligi Manchester City walilazimika kusubiri kabla ya kuwashinda nguvu Crystal Palace ambao hadi kufikia sasa hawajapata bao ama alama hata moja tangu msimu wa soka uanze.
City walikuwa mbele lakini sasa wanawaongoza majirani zao Manchester United kwa wingi wa mabao baada ya kuendeleza mwanzo mzuri msimu huu ambao umewafanya kufunga mabao 20 katika mechi nne zilizopita.
Walilazimika kusubiri hadi mwisho wa kindi cha kwanza kupata bao la kwanza dhidi ya kikosi cha Palace kilichoimarika, lakini The Eagles walipoteza mwelekeo baada ya kipindi cha kwanza huku City wakiinyeshea mvua ya mabao.

Leroy Sane akiifugia Manchester City dhidi ya Crystal PalaceHaki miliki ya pichaALAMY
Image captionLeroy Sane akiifugia Manchester City dhidi ya Crystal Palace

Leroy Sane alifunga bao la kwanza kufuatia pasi nzuri ya David Silva.
Raheem Sterling alifunga mabao mawili, Aguero akafunga bao la nne kabla ya Fabian Delph kufunga bao la tano.
Katika mechi kati ya Tottenham na West Ham, Harry Kane aliiweka mbele Tottenham na kuoongoza bao la pili naye Ericksen akafunga bao la tatu.

Harry Kane akiifungia Tottenham bao lake
Image captionHarry Kane akiifungia Tottenham bao lake

Lakini wakiwa na bao moja West Ham iliongeza bao la pili huku beki wa kulia Sergey Aurier wa Tottenhama akipewa kadi nyekundu kwa mchezo mbaya.
Hatahivyo harakati za West Ham za kutaka kusawazisha ziliambulia patupu baada ya mechi kukamilika 2-3.
Matokeo menginee:

Matokeo ya EPL
Image captionMatokeo ya EPL

Comments

Popular posts from this blog

Jifunze Jinsi ya kutengeneza sabuni ya Unga na ya maji

Mkataba wa Aishi Manura wavuja ukionyesha kujiunga na simba Simba

Antoine Griezmann: Nyota wa Atletico Madrid aomba radhi baada ya kujifanya mweusi