Iran yafanyia majaribio kombora lake
Iran inasema kuwa imefanyia majaribio kombora la Khorram-shahr.
Kombora hilo lilionyeshwa hadharani katika maonyesha ya kijeshi jana Ijumaa.
Iran imesema kuwa kombora hilo linaweza kusafiri mwendo wa kilomita 2,000.
Kituo cha runinga cha taifa hilo kilionyesha picha za sherehe hizo.
Kombora la kwanza la Khorram-Shahr lilirushwa angani Januari lakini likalipuka katikati ya mwendo.
Jaribio hilo lilifanywa siku chache baada ya Rais Trump wa Marekani kushambulia Iran katika hotuba yake katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
Rais wa Iran, Hassan Rouhani, ametetea hatua ya taifa lake kuimarisha zana zake kwa lengo la kujitetea.
Comments
Post a Comment