Hamilton ashinda michuano ya Singapore Grand Prix
Lewis Hamilton amefanikiwa kushinda michuano ya Singapore Grand Prix mbele ya mpinzani wake mkubwa Sebastian Vettel.
Licha ya kushinda,Hamilton anataja michuano ya mwaka huu kuwa na upinzani mkali.
Hamilton, ambaye alianza mzunguko wa tano kwa kusuasua aliongoza baada ya Vettel kugongana na dereva mwenzake wa Ferrari Kimi Raikkonen.
Zilikuwa ni mbio za aina yake, alisema Hamilton .
''Vettel alitarajiwa kushinda lakini kwa kutereza kwake basi nikawa mshindi''
Hamilton ameshinda kwa alama 28.
Comments
Post a Comment