Mwandishi kutoka Nigeria ashinda tuzo ya Komla Dumor

Amina Yuguda


Image captionAmina Yuguda ni mtangazaji katika kituo runinga cha eneo hilo cha Gotel

Mwandishi wa habari kutoka kaskazini mashariki mwa Nigeria ameshinda tuzo ya BBC la Komla Dumor.
Amina Yuguda ni mtangazaji katika kituo runinga cha eneo hilo cha Gotel, ambapo ameripoti kuhusu masuala kadha makuu ikiwemo kuhusu kundi la Boko Haram.
Yuguda atasafiri kwenda London kwa mafunzo ya miezi matatu mwezi Septemba.
Tuzo hili lilibuniwa kwa heshima ya Komla Dumor, mtangazaji wa runinga ya BBC ambaye alifariki ghafla akiwa na miaka 41 mwaka 2014.
Bi Yuguda amesema kuwa ushindi wake ni heshima kubwa.

Amina Yuguda
Image captionAmina Yuguda aliwavutia majaji kwa ripoti zake zinazohusu ushawishi wa radio nyumbani kwake.

Aliwavutia majaji kwa ripoti zake zinazohusu ushawishi wa radio nyumbani kwake.
"Kwa kisomo kidogo au kutokuwa na kisomo kabisa, wananchi wenzangu wanaelewa masula kadha ikiwemo uongozi wa Trump nchini Marekani, Korea Kaskania, Urusi chini ya Vladimir Putin na mengine mengi". Anasema Amina.
Mkurugenzi wa BBC World Service Group Francesca Unsworth, alisema Bi Yuguda alistahili ushindi huo.
Washindi wa awali wa tuzo la Kumla Dumor ni pamoja na mtangazaji raia wa Uganda Nancy Kacungira na mwandishi wa masuala ya biashara kutoka Nigeria Did Akinyelure

Comments

Popular posts from this blog

Jifunze Jinsi ya kutengeneza sabuni ya Unga na ya maji

Mkataba wa Aishi Manura wavuja ukionyesha kujiunga na simba Simba

Antoine Griezmann: Nyota wa Atletico Madrid aomba radhi baada ya kujifanya mweusi