Mbunge ambaye alihudhuria ndoa ya wapenzi wa jinsia moja ajiuzulu Israel
Mbunge mmoja nchini Israel amejiuzulu baada ya kukosolewa na vingozi wa dini kwa kuhudhuria ndoa ya wapenzi wa jinsia ya mpwa wake.
Yigal Guetta alifichua wakati wa mahojiano ya radio siku ya Jumapili kuwa alihudhuria harusi hiyo miaka miwili iliyopita.
Alisema kuwa licha ya ndoa ya njinsia kuwa kimyume na imani yake ya dini alitaka kumfurahisha mpwa wake.
Lakini viongozi watano wa dini walimkosoa Bw. Guetta kwa kuhujumu jina la Mungu na kutaka chama cha Shas kumfuta.
Kwenye mahojino na kituo cha radio cha Army, Bw. Guetta alieleza sababu zilizosababisha yeye ahudhurie harusi akisema nia yake ilikuwa ni kumfurahisha mpwa wake
Lakini barua iliyochapiswa siku ya Jumatatu na viongozi watano wa dini, ilisema kuwa ndoa ya jinsi moja ni kitu kibaya.
Bw. Guetta hakutoa taarifa rasmi baada ya kujiuzulu.
Comments
Post a Comment