Hospitali ya watoto ya Hunan nchini China yawafunda madaktari na wauguzi wa Zanzibar
Makamu wa Rais wa Hospitali ya Watoto ya Hunan nchini China akizungumza na washiriki wa mafunzo ya siku 10 ya Madaktari na wauguzi wanaoshughulikia watoto katika Hospitali ya Kivunge, Makunduchi na Mnazimmoja mafunzo yanayofanyika Mnazimmoja Mjini Zanzibar.
Balozi mdogo wa china aliepo Zanzibar XieXiawu akitoa hutuba katika ufunguzi wa mafunzo ya siku 10 ya kuwajengea uwezo madaktari na wauguzi wanaofanyakazi wodi za watoto za Hospitali ya Kivunge, Makunduchi na Kivunge.
Naibu Waziri wa Afya Harusi Said Suleiman akifungua mafunzo ya madaktari na wauguzi wanaoshughulikia watoto na kuimarisha utawala wa Hospitali, mafunzo yanayofanyika Hospitali kuu ya Mnazimmoja.
Washiriki wa mafunzo kutoka Hospitali ya Mnazimmoja, Kivunge na Makunduchi wakiwa pamoja na wakufunzi wao kutoka Hospitali ya Hunan China wakifuatilia hotuba ya ufunguzi iliyotolewa na Naibu Waziri wa Afya Bi. Arusi Said Suleiman (hayupo pichani).
Makamu wa Raiswa Hospitali ya watoto ya Hunan Chini China Zhu Lihui ameahidi kuwa Hospitali hiyo itaendelea kushirikiana na Hospitali ya Mnazimmoja ya Zanzibar kuwajengea uwezo wafanyakazi na kuimarisha Utawala wa Hospitali.
Zhu ameeleza hayo wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku kumi yanayowashirikisha madaktari na wauguzi 25 wanaoshughulikia watoto kutoka Hospitali ya Mnazimmoja, Kivunge na Makunduchi.
Amesema Hospitali ya watoto ya Hunan imewahi kutoa mafunzo kwa wafanyakazi 26 katika vipindi tofauti nchini China imeamua kufanya mafunzo Zanzibar kwa kushirikiana na Wizara ya Afya iliwafanya kazi wengi waweze kufaidika.
Ameeleza matarajio yake kuwa wafanyakazi waliopata nafasi ya kushiriki mafunzo hayo wataenda kuwaelimisha wafanyakazi wenzao ambao hawakubahatika kushiriki.
Aidha amesema kuja kwamadaktari bingwa kutoka jimbo la Hunan kutoa mafunzo hapa Zanzibar kutaongeza mashirikiano kati ya Hospitali ya Mnazimmoja na kubadilishana uzoefu katika kuimarisha afya za wananchi na kuimarisha masuala ya utawala.
Balozi mdogo wa China aliepo Zanzibar Xie Xiawu amesema ushirikiano baina ya China na Zanzibar niwamuda mrefu na nchi yake itaendelea kusaidia Zanzibar katika kuimarisha na kukuza maendeleo ya wananchi.
Alisema mafunzo yatakayotolewa na wataalamu kutoka Hospitaliya watoto ya Hunan yatawajengea uwezo watendaji wa wodi za watoto na kuimarisha afya ya mama baada ya kujifungua na watoto wanaozaliwa.
Akifungua mafunzo hayo yanayofanyika Hospitali mpya ya wazazi ya Mnazimmoja, Naibu Waziri wa Afya Harusi Saidi Suleiman aliishukuru Hospitali ya watoto ya Hunan kwa kusaidia kuwaongezea ujuzi wafanyakazi wanaoshughulikia matatizo ya watoto na kuimarisha utawalawa Hospitali.
Aliwataka washiriki wa mafunzo hayo kuwa wasikivu na kufuatilia kwa karibu masomo watakayo someshwa ili nao kuja kuwa walimu kwa wengine baada ya kumaliza na kuwawezesha wataalamu wa China kusomesha kada nyengine za afya.
Comments
Post a Comment