Tottenham na R Madrid zawika, Livepool yazuiwa

Harry Kane kwa sasa amefunga mabao 28 katika mechi zake 22 alizochzea klabu na taifa.


Haki miliki ya pichaREX FEATURES
Image captionHarry Kane kwa sasa amefunga mabao 28 katika mechi zake 22 alizochzea klabu na taifa.

Mshambuliaji Harry kane alifunga mabao mawili huku Tottenham ikiishinda Borussia Dortmund na hivyobasi kupiga jeki matumaini yao ya kombe la vilabu bingwa Ulaya katika uwanja wa Wembley.
Umahiri wa kane mbele ya goli ndio tofauti kubwa waliokuwa nayo Suprs ambao kwa kipindi kirefu cha mchezo huo walilazimika kulinda lango la kutokana na mchezo mzuri ulioonyeshwa na vijana wa Dortmund.
Bao lake la kwanza liliwawacha Dortmund bila jibu baada ya kutamba na mpira kutoka upande wa kushoto wa uwanja kabla ya kucheka na wavu dakika 15 katika kipindi cha kwanza baada ya bao la dakika ya 11 la Son Hueng-min kusawazishwa na mshambuliaji wa Dortmund Andriy Yarmolenko.
Bao la pili la Kane ulikuwa mkwaju wa kimo cha nyoka katika dakika ya sitini na hivyobasi kuipatia timu yake motisha ya kukabiliana na tishio la wapinzani wao waliotawala mechi hiyo.
Hatahivyo Tottenham walimaliza mechi hiyo wakiwa wachezaji 10 baada ya beki Jan Vertonghen kuonyeshwa kadi nyekundu kwa kumshika mchezaji wa ziada wa Dortmund Mario Gotze.
Matokeo mengine

Matokeo ya kombe la vilabu bingwa Ulaya
Image captionMatokeo ya kombe la vilabu bingwa Ulaya

Comments

Popular posts from this blog

Jifunze Jinsi ya kutengeneza sabuni ya Unga na ya maji

Mkataba wa Aishi Manura wavuja ukionyesha kujiunga na simba Simba

Antoine Griezmann: Nyota wa Atletico Madrid aomba radhi baada ya kujifanya mweusi