Saimon Msuva mchezaji bora wa Agosti
Mtanzania Saimon Msuva ametangazwa kuwa mchezaji bora wa Agosti katika klabu yake inayoshiriki Ligi Kuu ya Morocco.
Msuva ambaye anakipiga Difaa Al Jadid ameteuliwa kuwa mchezaji wa Agosti kutokakana na mchango wake mkubwa kwenye timu hiyo.
Msuva amejiunga na timu hiyo miezi miwili iliyopita akitokea Yanga ya Tanzania na tayari ameonekana kuwa tegemeo katika ufungaji wa mabao katika kikosi hicho.Msimu uliopita, Difaa Al Jadid ilishika nafasi ya pili, hivyo msimu huu itashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika.
Comments
Post a Comment