Arsenal yapata ushindi wa tatu mfululizo Yuropa
Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger amesema kuwa kikosi chake kilionyesha ujasiri huku kikiendeleza mwanzo mzuri wa kuwania kombe la Yuropa baada ya kupata ushindi wa 1-0 dhidi ya timu ya Crvena Zvezda huko Serbia.
Bao zuri la Olivier Giroud's katika dakika za lala salama ziliipatia Arsenal ushindi wa tatu mfululizo katika kombe hilo na hivyobasi kupnda hadi kilele cha kundi H wakiwa na alama tano juu ya BATE Borisov.
''Nadhani tuna ari ya kushinda '', alisema Wenger. ''hatukulaza damu nabtulitaka kupata nbao kila mara''.
Ujasiri wa wachezaji wa Arsenal ulijadiliwa wakati waliposhindwa 2-1 na Watford siku ya Jumamosi , huku mshambuliaji Troy Deeney akisema kuwa The Gunners hawana motisha.
Wenger alikiri kabla ya mechi hiyo kwamba matamshi hayo yalimuudhi , lakini akasema kuwa wachezaji wake watajibu kwa kuonyesha mchezo mzuri huko Serbia.
Comments
Post a Comment