Msimamo wa Acacia kuhusu makubaliano ya Barrick na Serikali
Kampuni ya uchimbaji madini nchini Tanzania, Acacia imesema kuwa inafahamu kuhusu serikali ya Tanzania na Barrick Gold Corporation (“Barrick”), kuwa wamefanya mkutano kwa ajili ya kushirikishana makubaliano yaliyofikiwa kutoka kwenye mazungumzo yaliyokuwa yakiendelea.
Mazungumzo hayo yalifanyika Ikulu Oktoba 19 kati ya serikali ya Tanzania na Barrick ambaye ndiye mwenye hisa kuwa (asilimia 64) katika Kampuni ya Acacia.
Katika taarifa yake iliyoitoa jana kwenye tovuti yao, Acacia wameeleza kuwa wamepata nakala ya makubaliano hayo, na kwa sasa wanatafuta ufafanuzi zaidi.
Acacia wameeleza kuwa hawakupewa taarifa yoyote rasmi kuhusu makubaliano hayo yaliyofikiwa kati ya pande hizo mbili na wao waweze kuyafikiria. Wameeleza kwamba, kama ambavyo walisema katika mkutano na waandishi wa habari kuwa, makubaliano yoyote yatakayofikiwa kati ya serikali na Barrick, ni lazima yaridhiwe na Acacia.
Aidha, wamesema watafikiria kuhusu makubaliano hayo mara watakapopata taarifa za kina zaidi, na ufafanuzi zaidi utatolewa muda muafaka.
Comments
Post a Comment