Wakuu wa zamani wa riadha wakamatwa kwa rushwa
Mkuu wa zamani wa wa shirikisho la riadha ulimwenguni Lamine Diack na mwanae Papa Massata wamekamatwa nchini Brazil kwa tuhuma za rushwa.
Tiyari wanashutumiwa kwa tuhuma kama hizo nchini Ufaransa kwa kupokea dola milioni 2 kwa ajili ya kuufanya mji wa Rio kuwa muandaaji wa michuano ya Olimpiki mwaka uliopita.
Lamin kwa sasa anashikiliwa nchini Ufaransa na tiyari amenyanganywa hati yake ya kusafiria huku Papa Massata akiwa amejificha nchini kwao Senegal.
Awali wawili hao walikana mashitaka ya kuhusika katika rushwa hiyo.
Comments
Post a Comment