Waingereza watupwa nje Luxembourg Open
Wacheza tennis waingereza Heather Watson na Naomi Brady kwa pamoja wametupwa nje ya michuano ya Luxembourg Open katika hatua ya robo fainali.
Watson namba mbili kwa ubora nchini Uingereza namba 81 duniani amepoteza kwa seti 6-4 6-4 mbele ya Elise Mertens wa Ubelgiji.
Kwa upande wa Naomi Broady amechapwa na Monica Puig wa Puerto Rico kwa seti 6-0 5-7 6-1.
Puig atakutana na Elise Mertens katika hatua ya nusu fainali na Pauline Parmentier wa Ufaransa atacheza na Caroline Witthoft wa Ujerumani.
Comments
Post a Comment