Xavi: Neymar alitaka kujiunga na PSG katika harusi ya Messi

Neymar baada ya kujiunga na PSG


Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionNeymar baada ya kujiunga na PSG

Nahodha wa zamani wa Barcelona Xavi amefichua kuwa Neymar alifichua habari za kutaka kujiunga na klabu ya PSG katika harusi ya Lionel Messi.
Ripoti za Neymar kutaka kuondoka Barcelona msimu uliopita na kuhusishwa kwake na PSG zilianza kubainika lakini zikashika kas,i na kufikia Agosti 3 Neymar alijiunga na PSG hadi 2022 kwa kitita kilichovunja rekodi ya dunia cha £198m.
Lakini kulingana na Xavi, Neymar alifichua mpango huo mwezi mmoja kabla katika harusi ya Lionel Messi wakati mshindi huyo wa mataji 5 ya mchezaji bora Ballon d'Or alipofunga ndoa na mpenziwe wa miaka mingi Antonella Roccuzzo nchini Argentina.
Raia huyo wa Brazil aliwaambia rafikize kuhusu azma yake ya kutaka kuondoka.
Akizungumza na BBC , Xavi ambaye aliichezea Barcelona mechi 700 na kushinda mataji 8 ya La Liga pamoja na makombe manne ya vilabu bingwa Ulaya alisema.
Alituambia siku ya harusi ya Messi kwamba anataka mabadiliko, alitaka kubadilisha klabu na tukamuuliza kwa nini?
Jibu lake alisema ,''kwa kweli sina raha Barcelona,ningependa kupata uzoefu tofauti Ulaya na PSG''.
''Ulikuwa uamuzi wake, lazime tuheshimu''.
''Na nadhani PSG ina kikosi kizuri chini Neymar, Mbappe na wana fursa nzuri ya kushinda kombe la vilabu bingwa Ulaya''.
Tangu uhamisho wake katika mji mkuu wa Ufaransa, Neymar amechezeshwa mechi zote na kufikia sasa amefunga mabao tisa na kutoa usaidizi wa mabao saba na anashirikiana vyema na Kylian Mbappe.
Wakati wa mechi ya klabu bingwa dhidi ya Anderlecht, wawili hao walitoa funzo kuhusu vile soka inavyochezwa.

Comments

Popular posts from this blog

Jifunze Jinsi ya kutengeneza sabuni ya Unga na ya maji

Mkataba wa Aishi Manura wavuja ukionyesha kujiunga na simba Simba

Antoine Griezmann: Nyota wa Atletico Madrid aomba radhi baada ya kujifanya mweusi