Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi apata ajali, avunjika mkono na Kulazwa hospitali ya KCMC

Mbunge wa Vunjo (NCCR-Mageuzi), James Mbatia amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC mjini Moshi baada ya kuvunjika mkono.

Mbatia ambaye pia ni mwenyekiti mwenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), amevunjika mkono wa kushoto baada ya kuteleza na kuanguka na amelazwa katika wodi za watu mashuhuri (VIP).

Msaidizi wa mbunge huyo, Hamis Hamis alisema jana Jumatano Desemba 20,2017 kuwa tukio hilo lilitokea juzi saa 2:45 usiku wakati akiondoka hotelini kurejea nyumbani.

Hamis alisema Mbatia alikuwa akishuka ngazi katika hoteli ya Uhuru iliyopo eneo la Shanty Town ndipo alipoteleza na kuanguka.

“Bahati nzuri pale kulikuwa na daktari wa KCMC anaitwa Ansbert Sweetbert ndiye alitoa huduma ya kwanza hadi kumpeleka KCMC,” alisema.

Alisema, “Kwa kweli huyo daktari alikuwa msaada mkubwa. Ndiye aliyempeleka KCMC na alikaa naye hadi saa nane usiku. Wauguzi na madaktari KCMC walimpa msaada mkubwa.”

Comments

Popular posts from this blog

GOR MAHIA MABINGWA WA SPORTPESA SUPER CUP 2017, SASA KUKIPIGA NA EVERTON JULAI 13

Marekani na Korea Kusini wafanya mazoezi ya pamoja ya jeshi

UKWELI KUHUSU MZEE MAJUTO, NA TETESI ZA KUFA