Trump awatishia watakaounga mkono maazimio ya UN juu ya mji wa Jerusalem

Trump


Image captionTrump;"Waache wapige Kura dhidi yetu. Tutahifadhi fedha yetu vya kutosha. Hatujali"

Rais wa Marekani, Donald Trump ametishia kusitisha misaada ya kifedha kwa nchi ambazo zinaunga mkono maazimio ya umoja wa mataifa ya kupinga Jerusalem kutambulika kama mji mkuu wa Israel.
Mapema mwezi huu, Bwana Trump alichukua uamuzi huo licha ya kukabiliwa na ukosolewaji mkubwa kutoka mataifa mbalimbali.
"Wanachukua mamia ya mamilioni ya dola na hata bilioni za dola kisha wanapiga kura dhidi yetu" aliwaambia wanahabari katika White House.
"Waache wapige Kura dhidi yetu. Tutahifadhi fedha yetu vya kutosha. Hatujali"
Maneno yake hayo yanakuja baada ya Mkutano wa Umoja wa mataifa kupiga kura kupinga hatua yoyote ya kuutambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel.

unHaki miliki ya pichaEPA
Image captionMkutano wa Umoja wa mataifa kupinga hatua yoyote ya kuutambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel.

Muswada wa maazimio haukuitaja Marekani lakini unasema maamuzi yoyote juu ya Jerusalem yanatakiwa kubatilishwa.
Mapema, Balozi wa Marekani katika Umoja wa mataifa Bi Nikki Haley aliwaonya wanachama wa umoja wa mataifa kuwa Rais Trump amemtaka kuwaripoti wale watakaopiga kura ya kuipinga Marekani.
Mji wa Jerusalem unaobishania una maeneo matakatifu ya dini tatu zenye kufuata imani ya Ibrahim - Uyahudi, Ukristo na Uislamu - sana maeneo mengi yanapatikana Jerusalem Mashariki.

TrumpHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMji wa Jerusalem

Israel ilitwaa eneo hilo kutoka Jordan wakati wa vita kati ya nchi za Kiarabu na Israel mwaka 1967 na imekuwa ikiuchukulia mji wote kuwa mji wake mkuu ambao hauwezi kugawanywa.
Jerusalem Mashariki hutazamwa kuwa mji mkuu wa taifa la Wapalestina (litakapoundwa) na mataifa ya Kiarabu na Kiislamu pamoja na Wapalestina wenyewe.

Trump
Image captionRamani inayoonyesha mji wa Jerusalem

Kwa mujibu wa maafikiano wakati wa mazungumzo ya amani ya Wapalestina na Waisraeli ya 1993, hatima ya mji huo ilifaa kuamuliwa wakati wa hatua za mwisho za mazungumzo.
Hatua ya Israel kudhibiti Jerusalem yote haijawahi kutambuliwa kimataifa na nchi zote zina afisi za kibalozi Tel Aviv.
Tangu 1967, Israel imejenga makazi kadha ya Wayahudi na kuna takriban walowezi 200,000 wa Kiyahudi eneo hilo. Makazi haya yamekuwa yakishutumiwa na jamii ya kimataifa

Comments

Popular posts from this blog

Jifunze Jinsi ya kutengeneza sabuni ya Unga na ya maji

Mkataba wa Aishi Manura wavuja ukionyesha kujiunga na simba Simba

Antoine Griezmann: Nyota wa Atletico Madrid aomba radhi baada ya kujifanya mweusi