Lema, Nassari wafurahia kupeleka ushahidi Takukuru
Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema amesema wamefurahia kauli ya mkurugenzi mkuu wa Takukuru kuwataka kupeleka ushahidi wa tuhuma zao kuwa kulikuwa na mchezo mchafu kushawishi madiwani wao kujiunga na CCM mbele ya Rais John Magufuli katika hafla ya kiserikali iliyofanyika jijini Arusha wiki iliyopita. Lema na mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari walidai kuwa madiwani wawili wa Chadema waliotangaza kujiunga na CCM wakati wa hafla ya kukabidhi kamisheni kwa maofisa wa Jeshi la Wananchi (JWTZ) kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, walishawishiwa kwa rushwa na kwamba kitendo hicho kilifanyika katika ofisi za Serikali na wanao ushahidi usio na shaka. Diwani mpya aliyeihama Chadema na kujiunga na CCM ni Rayson Ngowi wa Kata ya Kimandolu ambaye hata hivyo alikana kurubuniwa kufikia uamuzi huo. Walimuomba Rais Magufuli awaite ili wampatie ushahidi huo kuonyesha kuwa kitendo hicho ni kinyume na juhudi zake za kupambana na rushwa. Jana, Lema aliiambia Mwananc...