Posts

“SITAKI KUONA KIONGOZI WA DINI ANASUMBULIWA”- RC MAKONDA

Image
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Paul Makonda amewataka Viongozi wa Dini zote Waislam na Wakristo wenye matatizo yanayohitaji msaada wa Serikali ikiwemo Migogoro na Kesi kufika Ofisi kwake ili yaweze kupatiwa ufumbuzi. RC Makonda amesema hayo wakati wa Ibada ya uzinduzi wa Kanisa la KKKT Ubungo iliyoenda sambamba na Jubilee ya Miaka 500 ya Ujenzi wa Kanisa. Amesema kuwa Viongozi wa Dini wanafanya kazi kubwa ya kiroho katika kuijenga Jamii Bora hivyo hawapaswi kuzungushwa na Watendaji wa Serikali pale wanapohitaji kuhudumiwa kwakuwa thamani ya kazi wanayoifanya ni kubwa. “Mimi sio Mkuu wa Mkoa bali mimi ni Mtumishi wa Mungu katika Ofisi ya Mkoa wa Dar es salaam, Niwaombe Viongozi wote wa Dini Dar es Salaam sasa hivi msiangaike mkiwa na kesi kwenda kwa Wenyeviti wa Mtaa au Watendaji wa Mtaa, mkiwa na tatizo lolote njooni Ofisin kwangu, mimi ndio nitawatafuta hao, nisingependa kuona Kanisa au Msikiti wanasumbuliwa na Migogoro isiyoeleweka kwa misingi ya watu fula...

MAGAZETI YA LEO TZ NA NJE OKTOBA 20, 2017

Image

Msimamo wa Acacia kuhusu makubaliano ya Barrick na Serikali

Image
Kampuni ya uchimbaji madini nchini Tanzania, Acacia imesema kuwa inafahamu kuhusu serikali ya Tanzania na Barrick Gold Corporation (“Barrick”), kuwa wamefanya mkutano kwa ajili ya kushirikishana makubaliano yaliyofikiwa kutoka kwenye mazungumzo yaliyokuwa yakiendelea. Mazungumzo hayo yalifanyika Ikulu Oktoba 19 kati ya serikali ya Tanzania na Barrick ambaye ndiye mwenye hisa kuwa (asilimia 64) katika Kampuni ya Acacia. Katika taarifa yake iliyoitoa jana kwenye tovuti yao, Acacia wameeleza kuwa wamepata nakala ya makubaliano hayo, na kwa sasa wanatafuta ufafanuzi zaidi. Acacia wameeleza kuwa hawakupewa taarifa yoyote rasmi kuhusu makubaliano hayo yaliyofikiwa kati ya pande hizo mbili na wao waweze kuyafikiria. Wameeleza kwamba, kama ambavyo walisema katika mkutano na waandishi wa habari kuwa, makubaliano yoyote yatakayofikiwa kati ya serikali na Barrick, ni lazima yaridhiwe na Acacia. Aidha, wamesema watafikiria kuhusu makubaliano hayo mara watakapopata taarifa za...

Wema Sepetu Ataja Sababu Zilizomfanya Asiende Kumuona Tundu Lissu

Image
Mrembo wa Tanzania na Kada wa Chadema Wema Sepetu ametoa ya Moyoni kwa nini hakwenda kumuona mapema Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu baada ya kupigwa risasi septemba 7  ni kwamba asingeweza kumuona akiwa kwenye maumivu. Wema ameweka wazi maneno hayo kwenye ukurasa wake wa Instagram ikiwa ni baada ya dakika chache tangu kuachiwa kwa picha za kwanza za Mbunge huyo akiwa hospitali ya Nairobi nchini Kenya. Wema ameandika "Kisichokuua kinakufanya uwe na nguvuz zaidi....Utarudi tena ukiwa na nguvu kuliko ulivyokuwa awali...Shujaa wetu. ... Picha hii imenifanya nipate hisia. Sasa naweza andaa safari ya Nairobi kuja kukuona.. Awali nisingeweza kuvumilia kukuona ukiwa kwenye maumivu".  Wema Sepetu ametajwa na Chama cha  Chadema kama mmoja wa wahamasishaji  aliyeweza kuhamasisha watu kutoa michango kwa ajili ya matibabu ya Mbunge Tundu Lissu aliyelazwa Hospitali ya Nairobi baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana alipokuwa kwenye gari lake nje ya ma...

Waingereza watupwa nje Luxembourg Open

Image
Image caption Heather anashikilia nafasi ya 85 duniani Wacheza tennis waingereza Heather Watson na Naomi Brady kwa pamoja wametupwa nje ya michuano ya Luxembourg Open katika hatua ya robo fainali. Watson namba mbili kwa ubora nchini Uingereza namba 81 duniani amepoteza kwa seti 6-4 6-4 mbele ya Elise Mertens wa Ubelgiji. Kwa upande wa Naomi Broady amechapwa na Monica Puig wa Puerto Rico kwa seti 6-0 5-7 6-1. Puig atakutana na Elise Mertens katika hatua ya nusu fainali na Pauline Parmentier wa Ufaransa atacheza na Caroline Witthoft wa Ujerumani.

Wakuu wa zamani wa riadha wakamatwa kwa rushwa

Image
Image caption Papa Massata amesema tuhuma hizo ni sawa na fitina Mkuu wa zamani wa wa shirikisho la riadha ulimwenguni Lamine Diack na mwanae Papa Massata wamekamatwa nchini Brazil kwa tuhuma za rushwa. Tiyari wanashutumiwa kwa tuhuma kama hizo nchini Ufaransa kwa kupokea dola milioni 2 kwa ajili ya kuufanya mji wa Rio kuwa muandaaji wa michuano ya Olimpiki mwaka uliopita. Image caption Lamine Diack ameongoza shirikisho la riadha tokea mwaka 1999 mpaka 2015 Lamin kwa sasa anashikiliwa nchini Ufaransa na tiyari amenyanganywa hati yake ya kusafiria huku Papa Massata akiwa amejificha nchini kwao Senegal. Awali wawili hao walikana mashitaka ya kuhusika katika rushwa hiyo.