Posts

Tetesi za soka Ulaya Jumatatu 20.11.2017

Image
Image caption Mshambuliaji wa Uingereza na Tottenham Harry Kane, 24, Manchester City itashindana na Liverpool kumununua beki wa Southampton na Uholanzi Virgil van Dijk, 26, katika dirisha la uhamisho la Januari.{Daily Mirror}. City pia inataka kumsajili kiungo wa kati wa Schalke na Ujerumani Leon Goretzka ambaye kandarasi yake inakamilika mwishoni mwa msimu huu na amewavutia Arsenal, Liverpool na Chelsea (Daily Mirror) Mshambuliaji wa Uingereza na Tottenham Harry Kane, 24, anasema kuwa anapanga kuichezea Tottenham kwa kipindi chote cha mchezo wake kilichosalia (London Evening Standard) Image caption Daniel Sturridge Mshambuliaji wa Liverpool Daniel Sturridge, 28, yuko tayari kuondoka Liverpool ili kuweza kuchezeshwa na kuweza kuhifadhi nafasi yake katika timu ya Uingereza. (Daily Mirror) Barcelona inapanga kumnunua kiungo wa kati wa Arsenal na Ujerumani Mesut Ozil na inaweza kumuuza mchezaji wa Ureno Andre Gomes badala yake (Don Balon - in Spanish) Nahodha wa Paris S...

Generali Constantine Chiwenga aliyechukua mamlaka ya rais Mugabe

Image
Haki miliki ya picha AFP Image caption Generali Chiwenga alikuwa na mchango mkubwa katika kuendelea kumuweka madarakani Bwana Mugabe baada ya kushindwa katika uchaguzi dhidi ya mpinzani wake mkuu , Morgan Constantine Tsvangirai Generali Constantine Chiwenga, mwenye umri wa miaka 61, anasifiwa kama mkombozi wa kisiasa baada ya kuongoza mchakato wa jeshi wa kuchukua mamlaka nchini Zimbabwe,  Hata hivyo anakabiliwa na vikwazo vya Muunga wa Ulaya na Marekani kwa nafasi yake katika mateso dhidi ya upinzani na kuchukuliwa kwa mashamba ya wazungu. Raia wa Zimbabwe waliingia mitaani Jumapili kudai rais Robert Mugabe ajiuzulu huku wakiwa wameshikulia mabango yaliyoandikwa: " jeshi la Zimbabwe-sauti ya watu." Pastor Patrick Mugadza, alifanyiwa mateso na polisi mwenzi wa January mwaka huu kwa kutabiri kuwa Mugabe mwenye umri wa miaka 93- atakufa katika kipindi cha miezi tisa ijayo , na kwamba Mugabe alitaka kumpatia cheo cha Ujenerali mwanae wa kiume . Haki miliki ya picha...

Mugabe akabiliwa na kura bunge ya kutokuwa na imani nae

Image
Haki miliki ya picha EPA/THE HERALD Image caption Rais Mugabe anakabiliwa na shinikizo kutoka kwa umma na chama chake cha Zanu-PF Chama cha rais wa Zimbabwe Robert Mugabe kinatarajiwa kuanza mchakato wa kupiga kura ya kutokuwa na imani nae. Afisa wa Zanu-PF amesema kuwa hoja ya kumnyang'anya urais itawasilishwa bungeni leo Jumanne na mchakato wa kumg'oa madarakani unaweza kuchukua siku mbili tu. Mashtaka yaliyomo kwenye hoja hiyo ni pamoja na kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 93 "kumpa madaraka makubwa ya kikatiba mkewe Grace, na kushindwa kuheshimu katiba''. Viongozi wa kijeshi , ambao wiki iliyopita waliingilia kati kuchukua mamlaka ya nchi walisema atakutana na makamu wake wa rais wa zamani aliyeuhamishoni karibuni. Jeshi limesema kuwa lina mpango na Mugabe kuhusu hali ya baadae.  Jumapili , licha ya shinikizo kubwa Bwana Mugabe aliwashangaza wengi kwa kukataa kujiuzulu, na badala yake katika hotuma yake kupitia televisheni alisema kuwa ataong...

Juventus wachapwa baada ya kumpumzisha Gianluigi Buffon

Image
Haki miliki ya picha GETTY IMAGES Image caption Gianluigi Buffon (kati) amecheza mechi 627 Serie A , 20 nyuma ya rekodi ya Paolo Maldini Gianluigi Buffon aliachwa kwenye benchi Juventus walipokuwa wanacheza dhidi ya Sampdoria, hatua ambayo huenda iliwagharimu Jumapili. Walipokezwa kichapo cha 3-2. Buffon aliwekwa kwenye benchi pamoja na beki Andrea Barzagli, kwa sababu wanahitaji "muda kusahau" masaibu ya kukosa kufuzu kwa Kombe la Dunia. Massimiliano Allegri aliwapumzisha wawili hao, ambao tayari wamestaafu soka ya kimataifa, baada ya Italia kushindwa na Sweden mechi za muondoano wa kufuzu. Sampdoria waliongoza kupitia bao la kichwa la Duvan Zapata, Lucas Torreira na Gianmarco Ferrari nao wakaongeza na kufanya mambo 3-0. Gonzalo Higuain na nguvu mpya Paulo Dybala walikomboa mawili dakika za mwisho. Juventus wamesalia alama nne nyuma ya viongozi wa ligi Napoli ambao bado hawajashindwa. Inter Milan waliwapiku na kuingia nafasi ya pili baada ya kuwashinda At...

Benevento wavunja rekodi ya Manchester United

Image
Haki miliki ya picha GETTY IMAGES Image caption Benevento walikuwa tayari wamevunja rekodi ya kuwa na mwanzo mbaya zaidi Serie A Klabu ya Benevento nchini Italia imevunja rekodi ya Manchester United ya kuwa klabu iliyoanza msimu vibaya zaidi katika ligi mojawapo kati ya ligi tano kuu za soka Ulaya. Hii ni baada ya klabu hiyo kulazwa 2-1 muda wa ziada na Sassuolo. Limbukeni hao wa Serie A wameshindwa mechi zao 13 za kwanza kwenye msimu na hivyo wakavunja rekodi ya United ambao walishindwa mechi 12 mwanzo wa msimu wa 1930-31. Alessandro Matri aliwaweka Sassuolo kifua mbele lakini Samuel Armenteros akasawazisha kabla ya Gaetano Letizia alioneshwa kadi nyekundu upande wa Benevento. Domenico Berardi alipoteza penalti upande wa Sassuolo kabla ya Federico Peluso kuwafungia bao la ushindi. Benevento, ambao walifanikiwa kurejea Serie A mtawalia, walidhani wangepata alama yao ya kwanza ya msimu pale mkwaju wa penalti wa Berardi ulipogonga mwamba na kukosa kuingia. Matumaini yao...

Kansela Merkel awekwa njia panda

Image
Haki miliki ya picha REUTERS Image caption Kansela wa Ujerumani Angela Merkel Mazungumzo kuunda serikali ya mseto nchini Ujerumani yamevunjika, hali ambayo inaweka njia panda mstakabali wa Kansela Angela Merkel. Baada ya wiki nane ya majadiliano chama chenye mrengo wa kati cha Centrist Free Democrats -FDP- kimejitoa kikilalamikia tofauti zisizoweza kusuluhishwa na chama cha Merkel cha Christian Democrats na vyama vingine katika mazungumzo. Baadaye leo bibi Merkel atakutana na Rais wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier, ambaye ndiye mwenye nguvu kuitisha uchaguzi mpya. Bibi Merkel ameonya kuwepo kwa magumu katika wiki zijazo. Kiuhalisia makubaliano9 ya muungano huo yanawezekana lakini bado haijawa wazi iwapo kuna uwezekano wowote washiriki kufanya umuhimu wa kupata suluhu.

Mahakama ya Kenya kuamua juu ya kesi ya urais leo

Image
Haki miliki ya picha EPA Image caption Jaji Mkuu wa Mahakama ya juu zaidi nchini kenya David Maraga Mahakama ya juu zaidi nchini Kenya Jumatatu inatarajiwa kutoa uamuzi katika kesi zilizowasilishwa kwenye mahakama hiyo kupinga uchaguzi wa marudio wa tarehe 26 Oktoba ambapo rais wa sasa Uhuru Kenyatta alitangazwa kama mshindi.  Katika  K esi majaji watatakiwa kutoa uamuzi kuhusu masuala yafuatayo: Wataamua iwapo tume huru ya taifa ya chaguzi na mipaka (IEBC ) ilifaa kuteuwa upya wagombea urais au la. Uamuzi pia utatolewa na mahakama hiyo juu zaidi juu ya ya ikiwa kujiondoa kwenye uchaguzi huo kwa kiongozi Muungano wa upinzani Raila Odinga na Makamu wake Kalonzo Musyoka kuliathiri uchaguzi huo. Majaji pia watatoa uamuzi kuhusu ikiwa baada ya tume ya IEBC kushindwa kuendesha uchaguzi katika ameneo bunge 25 kati ya 290 kunahalalisha ama kubatilisha matokeo ya uchaguzi. Aidha Mahakama hiyo itawaeleza waKenya ikiwa tume ya uchaguzi (IEBC) ilikuwa na uwezo wa kuandaa uch...