Posts

Showing posts from September, 2017

DC WA KAKONKO KANALI NDAGALA APIGA MARUFUKU UNYANYASAJI KWA WAZEE,KUWATUHUMU WANAZUIA MVUA

Image
MKUU wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala amewaagiza Wananchi wa Wilaya ya Kakonko kuacha tabia ya kuwatuhumu baadhi ya wazee kuwa Wanazuia Mvua na kutaka kuwaondoa ikiwa ni pamoja na kuwauwa kwa kwa imani za kishirikina , na vikundi vitakavyo gundulika vinawatuhumu watachukuliwa hatua ili kukomesha vitendo hivyo. Akizungumza na Wananchi jana katika maadhimisho ya siku yaWazee Wilayani humo katika kijiji cha Kasanda ,Ndagala alisema kumekuwa na tabia ya Wananchi wengi kuwatuhumu baadhi ya wazee kuwa wanazuia mvua, jambo ambalo ni imani za kizamani na zilizopitwa na wakati.  "Kwa hiyo mimi nawaomba tuendelee kushirikiana na wazee wetu hawa kwa kuwa pia wana mchango wao mkubwa katika jamii,ni vyema tukawafanya wazee wetu waishi kwa amani na kuachana na imani hizo zinazoweza kuleta chuki na uhasama mkubwa baina yetu",alisema Ndagala. Alisema vitendo kama hivyo vilijitokeza mwaka jana, baadhi ya wazee walitaka kuuwawa kwa tuhuma hizo,aliema na kuongeza kuwa imani hiz...

ALIYEANDIKA UONGO WHATSAPP KUHUSU POLISI KUONEKANA HOSPITALI YA NAIROBI AFIKISHWA MAHAKAMANI!

Image
MKAZI  mmoja wa Kigamboni, Mbutusyo Mwakihaba (40), amefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kusambaza ujumbe katika mtandao kwamba kachero wa Usalama wa Taifa ameonekana jijini Nairobi karibu na hospitali aliyolazwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu. Mbutusyo amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa shtaka linalomkabili mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Victoria Nongwa. Wakili wa Serikali Janeth Magoho alidai mshtakiwa anakabiliwa na kosa la kusambaza taarifa za uongo chini ya kifungu namba 16 cha Sheria ya mtandao namba 4 ya mwaka 2015. Janeth amedai Septemba 11, mwaka huu kupitia mtandao wa ‘WhatsApp’ mshtakiwa aliandika “Huyu ni Kachero wa Usalama wa Taifa anatambulika kwa jina la Jose anaonekana Nairobi karibu na hospitali alikolazwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu…Mwaxcheni mwenzenu”. Mshtakiwa alikana kutenda makosa hayo, upelelezi wa kesi haujakamilika ambapo Hakimu Nongwa alikubali kumpa dhamana kwa masharti ya ...

Mikarafuu yateketea kwa moto Ziwani Pemba

Image
Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake Pemba, Rashid Hadid Rashid, akikaguwa  Shamba la Mikarafuu lilounguwa moto huko katika eneo la Semewani  Wilaya ya Chake Chake -Pemba. Miti 17 ya mikarafuu ambayo thamani yake bado haijulikana imeteketea  kwa moto huko bonde la Kijamvi  Shehia Semewani   Ziwani Wilaya ya Chake chake mkoa wa kusini PEMBA . Kwa mujibu wa watu walioshiriki kuzima moto huo wamesema chanzo chake  kilitokana na uvunaji wa asali. Akizungumzia kuhusu tukio hilo  mkuu wa wilaya ya chake chake Rashid Hadid Rashid amesema athari iliyopatikana sio ndogo kutokana na kutia unyonge kwa wenye  shamba hilo na pia ni hasara kwa taifa na kuwataka wananchi  kuwa makini katika matatizo kama hayo hasa kufua nyuki nyakati za usiku. Naye naibu sheha wa  shehia hiyo Khamis Suleiman Ali mara baadaya kuipata taarifa hiyo alichukua hatua ya kumpa taarifa sheha wa shehia hio ndipo taarifa ya tukio hilo ilipo enea na wananchi w...

Mshambuliaji wa ManCity Sergio Aguero ajeruhiwa katika ajali

Image
Haki miliki ya picha KAWILIKO MEDIA Mshambuliaji wa Manchester City Sergio Aguero amejeruhiwa katika ajali ya barabarani mjini Amsterdam, saa chache baada ya kuhudhuria tamasha. Raia huyo wa Argentina, mwenye umri wa miaka 29, anaarifiwa kuwa ndani ya taxi akielekea katika uwanja wa ndege baada ya kuhudhuria tamasha la muimbaji Maluma. City imesema "alikuwa Uholanzi katika siku yake ya mapumziko na amepata majeraha". Image caption Sergio Aguero Aguero anatarajiwa kurudi Manchester Ijumaa na atakaguliwa na kikosi cha madaktari wa City kabla ya kuelekea kwa mchuano wa Premier League watakapokaribishwa na Chelsea Jumamosi. Polisi Amsterdam wameithibitishia BBC kwamba watu wawili walikuwa ndaniya taxi iliyohusika katika ajali katika eneo la De Boelelaan mjini humo.

Mourinho: Pogba kukaa nje kwa muda mrefu

Image
Image caption Pogba baada ya kupata jeraha Jeraha la nyuma ya goti la kiungo wa kati wa Manchester United Paul Pogba's limemuweka nje kwa kipindi kirefu , kulingana na mkufunzi Jose Mourinho. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 aliumia na kutolewa nje dakika 19 za mechi ya vilabu bingwa kati ya The Reds na Fc Basel na tayari amekosa mechi nne zilizopita. ilidhaniwa kuwa Pogba kwamba mchezaji huo atakuwa nje kwa kati ya mwezi moja na wiki sita kufuatia jeraha hilo mnamo tarehe 12 mwezi Septemba. Mourinho hata hivyo hakuweza kutoa muda rasmi wa kurudi kwake. Mourinho alisema kuwa hazungumzii kuhusu majareha ya muda mrefu lakini alikuwa na matumaini makubwa kuhusu beki Phil Jones na Antonio Valencia. ''Siwezi kuwa na matumaini, kama vile Jones ama Valencia ninapowaona katika mazoezi na natumai kutakuwa na jibu'' ,aliongeza raia huyo wa Ureno. Kiungo wa kati Michael Carrick na Marouane Fellaini pia anatarajiwa kukosa mechi ya Jumamosi nyumbani dhidi...

Dele Alli apigwa marufuku kwa kuonyesha ishara ya kidole cha kati

Image
Haki miliki ya picha GETTY IMAGES Image caption Dele Alli apigwa marufuku kwa kuonyesha ishara ya kidole cha kati Kiungo wa kati wa Uingereza Dele Alli amepigwa marufuku kutoshiriki mechi moja ya kimataifa kufuatia hatua yake ya kuinua kidole cha kati wakati wa mechi ya kufuzu kwa kombe la dunia dhidi ya Slovenia. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 atashiriki mechi dhidi ya Lithuania siku ya Jumapili. Alli alisema kuwa ishara hiyo ilimlenga aliyekuwa mchezaji mwenza wa Spurs Kyle Walker wakati wa dakika ya 77 ya udhindi wa 2-1 katika kundi F. Kisa hicho kilitokea baada ya Alli kupigwa kumbo na beki wa Slovakia Martin Skrtel huku refa Clement Turpin akionyesha ishara ya mchezo uendelee. Ilionekana kana kwamba Alli alimuonyesha ishara hiyo ya kidole cha kati afisa huyo ambaye pia walirushiana maneno alipotolewa nje dakika ya 93.

Mapungufu ya UN katika mzozo wa Rohingya

Image
Haki miliki ya picha GETTY IMAGES Image caption Mamia kwa maelfu ya wakimbizi wa Rohingya wakiwa kambini Baghladesh Uchunguzi wa BBC umeibua maswali mazito kuhusiana na Umoja wa mataifa ulivyoshughulikia hali ya machafuko ya Rohingya. Nyaraka zilibainika na mahojiano yanaonyesha kuwa Umoja wa mataifa na serikali ya Myanmar waliwazuia maofisa waliokuwa wakiibua matatizo ya watu wa Rohingya dhidi ya serikali ya Burma. Maofisa wa umoja wa mataifa kwa mujibu wa uchunguzi wa BBC waliwazuia wafanyakazi wa haki za binadamu kuingia katika maeneo muhimu ili kutoa misaada. Haki miliki ya picha REUTERS Image caption Baadhi ya maeneo ya Rohingya Umoja wa mataifa wa Myanmar katika kuendelea kupinga uchunguzi wa BBC unasema kuwa umekuwa mstari wa mbele kusaidia raia, ambapo hata waliokimbia nchi walisaidiwa ulinzi na umoja wa mataifa na sasa wanaendelea kuhudumiwa katika katika kambi za wakimbizi. Hata hivyo vyanzo kutoka ndani ya umoja wa mataifa nchini humo vimeiambia BBC miaka mi...

Burundi hali si Shwari; Amnesty International

Image
Image caption Amnesty International limeonya juu ya usalama wa wakimbizi wa Burundi wanaorudi nchini kwao kutoka Tanzania Shirika la kimataifa linalotetea haki za binadamu la Amnesty International limeonya kuwa Maelfu ya wakimbizi wa Burundi wanaorudi nchini kwao kutoka Tanzania wanakabiliwa na hatari za kiusalama nchini mwao.  Mwezi uliopita, Tanzania, Burundi na shirika la umoja wa mataifa linalohudumia wakimbizi UNHCR walikubaliana kwamba kufikia mwisho wa mwaka huu wawe wamewarejesha wakimbizi elfu kumi na mbili wanaoishi Tanzania na wanataka kurudi kwao Burundi kwa hiari.  Lakini Amnesty International linasema, mpango huu unahatarisha maisha ya maelfu ya wakimbizi na linaamini kuwa wakimbizi wengi wanarejeshwa nyumbani kwao kutokana msukumo wa ushawishi kutoka serikali ya Tanzania na Burundi. Shirika hilo limedai kuwa hali ya usalama bado sio shwari katika ripoti yao inayotoka leo, wanasema visa vya kuteswa, kufungwa bila makosa, kubakwa na hata kuuwawa bado ...

Serikali ya Tanzania yalifungia gazeti la Raia Mwema kwa siku 90

Image
Image caption Raia Mwema limefungiwa na Serikali ya Tanzania Gazeti la Raia Mwema ambalo ni gazeti la kila wiki, limefungiwa na serikali ya Tanzania kwa siku 90 kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Idara ya Habari Maelezo. Idara hiyo imeeleza sababu za kusitisha uchapishaji na usambazaji wa gazeti hilo kuwa ni kutokana na kuchapishwa kwa toleo la tarehe 27 mwezi Septemba hadi 3 Oktoba 2017, lenye kichwa cha habari inayosomeka, "URAIS UTAMSHINDA JOHN MAGUFULI." Idara hio imedai kuwa gazeti hilo limetoa nukuu zisizo za ukweli kuhusu Rais John Magufuli, japo imekubali kuwa ni haki ya gazeti hilo kutoa maoni. Kusitishwa kwa gazeti hilo ni pamoja na toleo ya mtandaoni. Hili ni gazeti la tatu kufungiwa ndani ya miezi minne, ikiwemo gazeti la Mwana Halisi lilifungiwa takriban wiki mbili zilizopita kwa kile kilichodaiwa kuwa ni uchapishaji wa habari za uongo na kuchochea ambazo inadaiwa kuwa zinaweza kuhatarisha usalama wa taifa hilo. Hivi karibuni vyombo vya habari ...

Trump aapa ''kuikabili'' Korea Kaskazini ziarani bara Asia

Image
Haki miliki ya picha GETTY IMAGES Image caption Rais wa Korea Kusini Moon-Jae wakati wa mkutano na Trump mapema mwezi huu Rais wa Marekani Donald Trump atasafiri kuelekea katika mataifa matano ya bara Asia mnamo mwezi Novemba ili kushiriki katika mikutano ya kieneo, Ikulu ya Whitehouse imetangaza. Atazuru Japan, China, Korea Kusini, Vietnam, Ufilipino na Marekani ya Hawaii kwa ziara ya siku 11. Ziara hiyo ya marais itaimarisha harakati za kimataifa kukabiliana na tishio la Korea Kaskazini, taarifa hiyo ya Whitehouse imesema. Korea Kaskazini na Marekani zimekuwa zikirushiana cheche za maneno katika miezi ya hivi karibuni. Je maswala muhimu ya rais Trump katika mikutano hiyo yatakuwa nini katika ziara yake ya kwanza bara Asia? Taifa hilo ambalo limetengwa kiuchumi lilifanya jaribio lake la sita la kombora la kinyuklia mapema mwezi huu licha ya shutuma za kimataifa, imeahidi kufanya jaribio jingine katika bahari ya pacific. Image caption Rais Kim Jong Un na majenerali wa...

MAGAZETI YA TZ NA NJE SEPT 28,2017

Image