Mourinho: Pogba kukaa nje kwa muda mrefu


Pogba baada ya kupata jeraha


Image captionPogba baada ya kupata jeraha

Jeraha la nyuma ya goti la kiungo wa kati wa Manchester United Paul Pogba's limemuweka nje kwa kipindi kirefu , kulingana na mkufunzi Jose Mourinho.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 aliumia na kutolewa nje dakika 19 za mechi ya vilabu bingwa kati ya The Reds na Fc Basel na tayari amekosa mechi nne zilizopita.
ilidhaniwa kuwa Pogba kwamba mchezaji huo atakuwa nje kwa kati ya mwezi moja na wiki sita kufuatia jeraha hilo mnamo tarehe 12 mwezi Septemba.
Mourinho hata hivyo hakuweza kutoa muda rasmi wa kurudi kwake.
Mourinho alisema kuwa hazungumzii kuhusu majareha ya muda mrefu lakini alikuwa na matumaini makubwa kuhusu beki Phil Jones na Antonio Valencia.
''Siwezi kuwa na matumaini, kama vile Jones ama Valencia ninapowaona katika mazoezi na natumai kutakuwa na jibu'' ,aliongeza raia huyo wa Ureno.
Kiungo wa kati Michael Carrick na Marouane Fellaini pia anatarajiwa kukosa mechi ya Jumamosi nyumbani dhidi ya Crystal Palace.

Comments

Popular posts from this blog

Jifunze Jinsi ya kutengeneza sabuni ya Unga na ya maji

Mkataba wa Aishi Manura wavuja ukionyesha kujiunga na simba Simba

Antoine Griezmann: Nyota wa Atletico Madrid aomba radhi baada ya kujifanya mweusi