Trump aapa ''kuikabili'' Korea Kaskazini ziarani bara Asia

Rais wa Korea Kusini Moon-Jae wakati wa mkutano na Trump mapema mwezi huu


Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionRais wa Korea Kusini Moon-Jae wakati wa mkutano na Trump mapema mwezi huu

Rais wa Marekani Donald Trump atasafiri kuelekea katika mataifa matano ya bara Asia mnamo mwezi Novemba ili kushiriki katika mikutano ya kieneo, Ikulu ya Whitehouse imetangaza.
Atazuru Japan, China, Korea Kusini, Vietnam, Ufilipino na Marekani ya Hawaii kwa ziara ya siku 11.
Ziara hiyo ya marais itaimarisha harakati za kimataifa kukabiliana na tishio la Korea Kaskazini, taarifa hiyo ya Whitehouse imesema.
Korea Kaskazini na Marekani zimekuwa zikirushiana cheche za maneno katika miezi ya hivi karibuni.
Je maswala muhimu ya rais Trump katika mikutano hiyo yatakuwa nini katika ziara yake ya kwanza bara Asia?
Taifa hilo ambalo limetengwa kiuchumi lilifanya jaribio lake la sita la kombora la kinyuklia mapema mwezi huu licha ya shutuma za kimataifa, imeahidi kufanya jaribio jingine katika bahari ya pacific.

Rais Kim Jong Un na majenerali wake wa jeshi
Image captionRais Kim Jong Un na majenerali wake wa jeshi

Katika hotuba kwa Umoja wa Mataifa, bwana Trump ameahidi kuiangamiza Korea Kaskazini akisema kuwa kiongozi wa taifa hilo Kim Jong-Un ''anajihatarisha''.
Katika taarifa isiokuwa ya kawaida bwana Kim aliapa kumkabili rais huyo wa Marekani aliyedai kuwa na ''akili punguani kwa vita''.
Bwana Trump ataomba kuungwa mkono na majirani wa taifa hilo ikiwemo China kuendeleza vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Korea Kaskazini.

Comments

Popular posts from this blog

Jifunze Jinsi ya kutengeneza sabuni ya Unga na ya maji

Mkataba wa Aishi Manura wavuja ukionyesha kujiunga na simba Simba

Antoine Griezmann: Nyota wa Atletico Madrid aomba radhi baada ya kujifanya mweusi