Mikarafuu yateketea kwa moto Ziwani Pemba
Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake Pemba, Rashid Hadid Rashid, akikaguwa Shamba la Mikarafuu lilounguwa moto huko katika eneo la Semewani Wilaya ya Chake Chake -Pemba.
Miti 17 ya mikarafuu ambayo thamani yake bado haijulikana imeteketea kwa moto huko bonde la Kijamvi Shehia Semewani Ziwani Wilaya ya Chake chake mkoa wa kusini PEMBA .
Kwa mujibu wa watu walioshiriki kuzima moto huo wamesema chanzo chake kilitokana na uvunaji wa asali.
Akizungumzia kuhusu tukio hilo mkuu wa wilaya ya chake chake Rashid Hadid Rashid amesema athari iliyopatikana sio ndogo kutokana na kutia unyonge kwa wenye shamba hilo na pia ni hasara kwa taifa na kuwataka wananchi kuwa makini katika matatizo kama hayo hasa kufua nyuki nyakati za usiku.
Naye naibu sheha wa shehia hiyo Khamis Suleiman Ali mara baadaya kuipata taarifa hiyo alichukua hatua ya kumpa taarifa sheha wa shehia hio ndipo taarifa ya tukio hilo ilipo enea na wananchi wa shehia hio kusaidia kuuzima moto huo.
Hata hivyo amewapongeza wananchi hao kwa mashirikiano yao katika kukabiliana na tatizo hilo.
Kwa Upande wake Mussa Hamad Shaame amesema amesikitika sana kwa tukio hilo kwani hiyo ni kudra ya Mwenyezi Mungu lakini watu wanapofanya kazi kama hizo wasichoke kuchukua tahadhari ili kunusuru maafa yasitokee.
Shamba hilo linamilikiwa na Saleh Hamad Said , Abdalla Mussa na Biziada Othman Yussuf.
Comments
Post a Comment