Mapungufu ya UN katika mzozo wa Rohingya
Uchunguzi wa BBC umeibua maswali mazito kuhusiana na Umoja wa mataifa ulivyoshughulikia hali ya machafuko ya Rohingya.
Nyaraka zilibainika na mahojiano yanaonyesha kuwa Umoja wa mataifa na serikali ya Myanmar waliwazuia maofisa waliokuwa wakiibua matatizo ya watu wa Rohingya dhidi ya serikali ya Burma.
Maofisa wa umoja wa mataifa kwa mujibu wa uchunguzi wa BBC waliwazuia wafanyakazi wa haki za binadamu kuingia katika maeneo muhimu ili kutoa misaada.
Umoja wa mataifa wa Myanmar katika kuendelea kupinga uchunguzi wa BBC unasema kuwa umekuwa mstari wa mbele kusaidia raia, ambapo hata waliokimbia nchi walisaidiwa ulinzi na umoja wa mataifa na sasa wanaendelea kuhudumiwa katika katika kambi za wakimbizi.
Hata hivyo vyanzo kutoka ndani ya umoja wa mataifa nchini humo vimeiambia BBC miaka mine iliyopita kabla ya mzozo huu wa sasa, mkuu wa Umoja wa mataifa wa Myanmar raia wa Canada Renata Lok Dessallin alizuia makundi ya wanaharakati wa haki za binadamu kufika katika maeneo ya Rohingya.
Pia alijaribu kuzuia uhamasishaji kuhusiana na vurugu za eneo hilo pamoja na kuwaondoa wafanyakazi waliojaribu kutuliza mzozo huo kwa kuendesha mikutano na makongamano.
Zaidi ya watu laki tano wa Rohingya wamekimbilia nchi jirani ya Bangladesh.
Comments
Post a Comment