Posts

Tamko la Serikali kuhusu homa ya Ini,

Image
Serikali imesema kuwa inatarajia kuanza kutoa Chanjo ya Homa ya Ini kwa wananchi wote bila kujali kigezo cha umri wala uwezo wa kifedha kwa wale wote wenye dalili za ugonjwa  au wenye ugonjwa wa Ini. Hayo yamesemwa jana jijini Dar es salaam na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu alipokuwa akizungumza kuhusu maadhimisho ya ugonjwa wa homa ya ini duniani. “Katika kuadhimisha siku ya ugonjwa wa homa ya ini duniani tumedhamiria kuhakikisha chanjo ya ugonjwa huu inapatikana kwa watu wote nchini ambao wana hatari ya kupata maambukizi ya homa ya ini au tayari wamepata ugonjwa huo, watapata chanjo kwa bei nafuu kwa mswaka wa bajeti 2018/2019”  alisema Ummy. Alisema kuwa ili kujilinda na maambukizi ya ugonjwa wa homa ya ini mpango wa damu salama unatakiwa kuhakikisha wanapima damu zote za wachangiaji kabla ya kuwawekea wagonjwa wanaohitaji huduma ya damu. Aidha, Ummy alisema kuwa asilimia 50 ya wanaotumia madawa ya kulevya kwa kujidunga s...
Image
Tundu Lissu Kaachiwa Kwa Dhamana Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA) na Rais wa Chama cha Mawakili  Tanzania , Mhe. Tundu Lissu ameachiwa kwa dhamana ya Milioni 10 leo katika kesi yake iliyokuwa inamkabili ya uchochezi. Mahakama ya Kisutu imempa dhamana Mh Tundu Lissu kwa sharti la kuwa na wadhamini wawili watakaosaini dhamana ya thamani ya milioni kumi. Aidha, Mahakama hiyo pia imemtaka Tundu Lissu kutokuondoka nje ya jiji la Dar es Salaam bila kuwa na kibali maalum cha mahakama. Uamuzi huo umetolewa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu Jijini Dar es Salaam, Wilbard Mashauri. Upande wake Tundu Lissu alikuwa anatetewa na jopo la mawakali 18 likiongozwa na Fatma Karume na Peter Kibatala ambapo katika shauri la kwanza waliomba Mahakama impe dhamana mteja wao. Tundu Lissu alitiwa katika mikono ya dola mnamo Julai 20 siku ya Alhamsi katika uwanja wa ndege akiwa anaelekea nchini Rwanda. na siku iliyofuata  jeshi hilo lilikwenda kufanya upekuzi nyumbani kwa ...

FLORA Mbasha na Emmanuel Mbasha Watakiwa Kuacha Utoto...Kisa Kizima Hichi Hapa

Image
Hakuna kazi ngumu kama kutoa ushauri kwa watu wenye mgogoro unaohusisha uhusiano wa kimapenzi, kwa sababu ni lazima upande mmoja utachukia, kwani ili kitu kiwe kizuri, ni lazima uwe mkweli kwa asilimia mia moja. Ni lazima mmoja atachukia kwa sababu siku zote katika uhusiano wa kimapenzi, upande mmoja unakosea. Barua yangu ya leo inawaelekea kaka na dada yangu, Emmanuel Mbasha na aliyekuwa mkewe, Flora, siku hizi akifahamika kama Madam Flora. Dada yangu Flora, ninamkubali tangu alipoanza kufanya vyema na Wimbo wa Jipe Moyo, Majaribu na nyinginezo. Dada Flora, wewe ni mtumishi wa Mungu, kama unaamini kuwa majaribu ni kipimo kwa mtu aliyeokoka, kwa nini unashindwa kumaliza bifu lenu kimya kimya ukizingatia kila mtu kwa sasa ana maisha yake mapya? Hii ni kwa sababu ya ule unaodaiwa kuwa ujumbe wako kusambaa ambao ulimsema vibaya mumeo wa zamani, kwamba alikuwa chanzo cha kuachana kwenu. Pengine maisha ya kistaa yamewaathiri au labda huenda bado mnapendana, lakin...

Sheria Tano Za Fedha Unazopaswa Kuzijua Na Kuzisimamia Kama Unataka Kuondoka Kwenye Umasikini.

Moja ya vitabu nilivyowahi kusoma kuhusu fedha na nikavielewa na hata kujenga msingi wangu wa kifedha ni kitabu   THE RICHEST MAN IN BABYLON.   Kitabu hichi kimetoa elimu muhimu sana kuhusu fedha kwa kutumia hadithi ya enzi za utawala wa Babeli. Kitabu hichi kimeeleza kwa kina kuanzia kuongeza kipato, kuweka akiba, kuwekeza, kuondoka kwenye madeni, kulinda utajiri na mengine muhimu.   Kwenye kitabu hichi, ipo hadithi ya mtu mmoja tajiri, ambaye baada ya kijana wake kufikia umri wa kuweza kujitegemea, alimwita na kumwambia anataka ampime na kuona kama anaweza kurithi mali zake. Na alimpa mfuko wa fedha, pamoja na kitabu cha sheria za fedha, na kumwambia miaka kumi ijayo, arudi kwake na kumwambia amefanya nini na fedha zile.  Kama ilivyo kwa wengi wanaopata fedha nyingi kwa wakati mmoja, hakuhangaika na zile sheria za fedha, badala yake alianza kutumia fedha zile. Alishauriwa kujihusisha na biashara asizozielewa, mojawapo ikiwa ni kamari na kupoteza fedha zote. B...

USHAURI; Jinsi Ya Kuepuka Kusumbuliwa Na Watu Unaowakopesha Wakiwa Na Shida.

Karibu kwenye makala yetu ya leo ya USHAURI WA CHANGAMOTO ambazo zinatuzuia kufikia mafanikio makubwa kwenye maisha yetu. Changamoto ni sehemu ya maisha yetu ya kila siku, na tunapaswa kuzivuka ili kuweza kufika kule tunakotaka kufika. Lakini wakati mwingine changamoto zinakuwa kubwa kiasi kwamba tunashindwa kujua tuchukue hatua gani. Hapa ndipo tunashirikiana kuhakikisha tunasaidiana kutatua changamoto.  Kwenye makala ya leo tunaangalia changamoto ya watu kukukopa fedha, halafu wanakuwa wagumu kukulipa. Kama wahenga walivyosema, kukopa huwa ni harusi, lakini kulipa ni matanga. Watu wanapokuwa wanakopa wanakuwa wanyenyekevu na wazuri sana, lakini unapofika wakati wa kulipa ndipo huonesha tabia zao halisi, wanakuwa wasumbufu mno. Hii ni changamoto kubwa kwa mafanikio, kwa sababu iwapo watu unaowakopesha ni wa karibu, wanakuwa mzigo kwako na wakati mwingine unaharibu hata mafanikio.  Kwenye makala ya leo tutaangalia jinsi ya kuondokana na changamoto hii. Ila kwanza tuanze na...

AMPIGA RISASI BABA MKWE WAKE KANISANI

Image
Chanzo cha mwandishi wa habari wa kujitegemea, Elias Mhegera kumpiga risasi baba mkwe wake kanisasni juzi ni hisia kuwa mzazi wa mwanamke huyo ndiye chanzo cha kuvunjika kwa ndoa yao miaka 10 iliyopita. Mhegera ambaye kwa sasa anashikiliwa na Jeshi la Polisi tangu juzi amekuwa katika mvutano na mke wake ambaye waliachana miaka 10 iliyopita. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni amethibitisha kutokea kwa tukio hilo juzi majira ya saa1:30 asubuhi katika Parokia ya Bikira Maria, Kibangu na kueleza kuwa chanzo ni ugomvi wa kifamilia. “Adrian Mpande alijeruhiwa bega la kushoto na mtu anayedaiwa kuwa ni mkwe wake. Uchunguzi wa awali umebainisha kuwa sababu ni mambo ya kifamilia,” alisema Kamanda Kaganda na kuongeza: “Tunaendelea na uchunguzi na kukiwa na umuhimu tutawaeleza kwa uwazi. Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo ambaye hakutaka jina lake litajwe alisema kuwa Mzee Mpande alipigwa risasi mbili wakati akijiandaa kuingia kanisani kwa ibada juzi Jumapili.

Msuva ajitokeza mazoezini na kuaga rasmi viongo wa Yanga SC

Image
Kiungo mshambuliaji wa timu ya taifa ya Tanzania na Yanga SC, Saimon Happygod Msuva amewaaga rasmi wachezaji wenzie wanachama na mashabiki wa klabu hiyo Msuva mabaye ni mfungaji bora wa ligi kuu ya Vodaco Tanzania Bara amefanya hivyo leo baada ya kujitokeza katika mazoezi ya timu hiyo yaliyokuwa yakifanyika uwanja wa Uhuru Kiungo huyo muhimu wa Yanga SC anakwenda nchini Morocco kujiunga na timu ya Difaa al Jadida  ambayo imeridhia kuwalipa wana jangwani hao kiasi cha dola 80,000 (Sh milioni 177) kwa kandarasi ya miaka mitatu. Akizungumzia suala la kuaga na safari yake Msuva alisema; “Kwanza kabisa nimshukuru mwenyezi mungu kwa kunipatia timu nje ya nchi japo ni ndani ya bara letu ila wenzetu wameendelea (advance) sana kwa hiyo naona ni mahali sahihi kwangu na ni hatua pia kwangu”. Simon Msuva ameendelea kwa kusema “pili niwashukuru mashabiki wa timu yangu kwa kuwa nami muda wote niliokuwa na timu ya Yanga pia niwashukuru watanzania wote kwa kuendelea kuutambua mchango wangu ...